Iraq

Iraq (kwa Kiarabu العراق, al-ʿIrāq) ni nchi ya Asia ya Magharibi inayokaliwa hasa na Waarabu (75-80%) lakini pia na wengine, hasa Wakurdi 15%).

Iraq
Iraq
Ramani ya Iraq

Inajumlisha eneo la Mesopotamia pamoja na sehemu ya jangwa la Shamu na ya milima ya Zagros.

Imepakana na Kuwait, Saudia, Yordani, Syria, Uturuki na Uajemi. Kuna pwani fupi kwenye Ghuba ya Uajemi.

Jiografia

Sehemu kubwa ya Iraq ni jangwa lakini kuna eneo lenye rutuba kati ya mito ya Frati na Hidekeli.

Kaskazini ni hasa nchi ya milima inayopanda hadi ya kimo cha m 3,611 juu ya UB.

Hali ya hewa inalingana na mazingira. Kipindi cha kiangazi kuna joto kali. Majira ya Desemba-Februari kuna halijoto ya kupoa kusini na baridi kali mlimani.

Historia

Iraq ni nchi yenye historia ndefuː ilikuwa kitovu cha ustaarabu wa binadamu, mahali pa miji ya kwanza duniani katika Sumeri na Babeli.

Baada ya kusambaratika kwa milki ya Waturuki Waosmani walioitawala muda mrefu, Iraq ilikubaliwa kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mataifa mwaka 1932 ingawa hali halisi ilikuwa nchi lindwa chini ya athira ya Uingereza hadi mwaka 1958.

Miaka ya hivi karibuni imejulikana hasa kutokana na vita mbalimbaliː kwanza vita dhidi ya Uajemi chini ya serikali ya Saddam Hussein tangu 1981, baadaye vita dhidi ya Kuwait na Marekani.

Vita vya pili vya ghuba ya 2003 iliyoleta uvamizi wa Marekani ilizidi kuleta vifo na uharibifu.

Hatimaye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoingiliwa na DAESH iliyoteka sehemu kubwa ya nchi, hasa kaskazini na magharibi, hadi mwishoni mwa mwaka 2017.

Watu

Lugha rasmi na ya kwanza ni Kiarabu, ikifuatwa na Kikurdi ambayo pia imekuwa lugha rasmi, halafu lugha nyingine za jamii mbalimbali ambazo pengine zinatambulika kieneo.

Wakazi wengi (95%), hasa baada ya vita vya hivi karibuni, ni Waislamu, wakiwemo kwanza Washia halafu na Wasuni. Wakristo waliobaki ni 5%, wakiwemo hasa waamini wa Kanisa Katoliki la Wakaldayo na Waashuru wa Kanisa la Mashariki.

Uchumi

Iraq ina akiba kubwa za mafuta ya petroli ardhini. Mapato kutokana na mafuta yalileta maendeleo makubwa nchini hadi mwanzo wa kipindi cha vita vilivyoharibu sana nchi pamoja na uchumi wake.

Tazama pia

Marejeo

  • Shadid, Anthony 2005. Night Draws Near. Henry Holt and Co., NY, U.S. ISBN 0-8050-7602-6
  • Hanna Batatu, "The Old Social Classes and the Revolutionary Movements of Iraq", Princeton: Princeton University Press, 1978
  • Charles Glass, "The Northern Front: A Wartime Diary"' Saqi Books, London, 2004, ISBN 0-86356-770-3
  • A Dweller in Mesopotamia Archived 25 Mei 2005 at the Wayback Machine., being the adventures of an official artist in the garden of Eden, by Donald Maxwell, 1921. (a searchable facsimile at the University of Georgia Libraries; DjVu & layered PDF Archived 6 Septemba 2005 at the Wayback Machine. format)
  • By Desert Ways to Baghdad Archived 2 Aprili 2005 at the Wayback Machine., by Louisa Jebb (Mrs. Roland Wilkins) With illustrations and a map, 1908 (1909 ed). (a searchable facsimile at the University of Georgia Libraries; DjVu & layered PDF Archived 6 Septemba 2005 at the Wayback Machine. format)
  • 2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  • Benjamin Busch, "'Today is Better than Tomorrow'. A Marine returns to a divided Iraq", Harper's Magazine, October 2014, pp. 29–44.

Viungo vya nje

Iraq 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Serikali
    Taarifa za jumla
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Iraq  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Iraq kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Iraq JiografiaIraq HistoriaIraq WatuIraq UchumiIraq Tazama piaIraq MarejeoIraq Viungo vya njeIraqAsia ya MagharibiWaarabuWakurdi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UendelevuJinaMkanda wa jeshiVichekeshoNdovuUpendoUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaNdoaNikki wa PiliChakulaAlama ya uakifishajiUtataAmina ChifupaTungoMkoa wa KilimanjaroOrodha ya Marais wa BurundiPemba (kisiwa)MaadiliMbwana SamattaDhima ya fasihi katika maishaFamiliaJiniDolar ya MarekaniLatitudoMfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania22 ApriliMazoezi ya mwiliRayvannyUnyevuangaUfinyanziKaswendeDodoma MakuluKizunguzunguIsraelVitenzi vishirikishi vikamilifuLa LigaAsidiMarekaniUfugaji wa kukuSexMfumo wa nevaMuungano wa Tanganyika na ZanzibarHistoria ya AfrikaTeknolojiaUlayaWanyaturuDhanaUturukiPasaka ya KikristoWilaya za TanzaniaNduniRitifaaHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoFasihi andishiTafsidaPentekosteMtaalaDubuMauaji ya kimbari ya RwandaJoseph ButikuLughaHistoria ya WapareUajemiOrodha ya milima mirefu dunianiMkataba wa Helgoland-ZanzibarRiwayaWikipedia ya KiswahiliMatendo ya MitumeUnyagoUsafi wa mazingiraWazaramoBunge la TanzaniaTahajiaViwakilishi vya sifaKilimanjaro (volkeno)Mkoa wa TaboraMsongola🡆 More