Uthai

Uthai (pia: Siam, Thailand, Tailandi, Thailandi, Tailendi) ni ufalme katika Asia ya Kusini-Mashariki.

Uthai

Imepakana na Laos, Kambodia, Malaysia na Myanmar.

Ina pwani kwenye Ghuba ya Uthai ya Bahari ya Kusini ya China upande wa kusini na Bahari Hindi upande wa magharibi.

Nchi ina wakazi zaidi ya milioni 67, hivyo inashika nafasi ya 20 duniani.

Mji mkuu na mji mkubwa ni Bangkok (ukiwa na wakazi milioni 8).

Historia

Uthai ilikuwa nchi pekee ya Asia Kusini Mashariki iliyofaulu kukwepa ukoloni.

Nchi iliitwa rasmi 'Siam (สยาม) hadi mwaka 1939, tena kati ya 1945 na 1949.

Neno Thai (ไทย) linamaanisha "uhuru" kwa Kithai ni pia jina la kundi kubwa la watu nchini ambao ni Wathai (75-85%), mbali na Wathai-Wachina (12%).

Tangu tarehe 19 Septemba 2006 nchi imetawaliwa na kamati ya jeshi. Jeshi ilipindua serikali ya waziri mkuu Thaksin Shinawatra bila kumwaga damu. Viongozi wa kijeshi walipatana na mfalme kwamba wataandaa uchaguzi mpya.

Lakini hata baada ya chaguzi huru kadhaa nchi haijatulia kisiasa.

Watu

Nchini Uthai kuna lugha za asili 73 (angalia orodha ya lugha za Uthai). Kati yake, Kithai ndiyo lugha rasmi.

Wathai walio wengi (94.5%) hufuata dini ya Ubuddha katika madhehebu ya Theravada. Kusini, mpakani kwa Malaysia, kuna Waislamu (4.3%). Wakristo ni 1.2%.

Tazama pia

Viungo vya nje

Uthai 
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Serikali
    Taarifa za jumla
    Utalii
  1. Thailand travel dictionary
    Vingine
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Uthai  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uthai kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Uthai HistoriaUthai WatuUthai Tazama piaUthai Viungo vya njeUthaiAsia ya Kusini-MasharikiUfalme

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Umoja wa MataifaShinikizo la ndani ya fuvuSerikaliHofuMachweoMaana ya maishaAslay Isihaka NassoroAzimio la ArushaKuraniMishipa ya damuKanisa KatolikiTarakilishiMfumo wa upumuajiMsambaMtume PetroBahari ya ShamuBunge la TanzaniaMalariaTupac ShakurWahangazaMuda sanifu wa duniaWanyama wa nyumbaniUshairiMisimu (lugha)Manabii WadogoMofolojiaAfrika KusiniKigoma-UjijiKunguniHistoria ya WapareOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaOrodha ya milima mirefu dunianiMzabibuWamanyemaMafarisayoNguruweHafidh AmeirLugha ya maandishiWagogoMichezo ya watotoMweziLughaVielezi vya wakatiAdhuhuriKunguruMauaji ya kimbariShetaniUkristoKilomitaKiingerezaMungu ibariki AfrikaMkoa wa MwanzaNguruwe-kayaSomalilandMagonjwa ya kukuWaziri wa Mambo ya Ndani (Tanzania)Uzazi wa mpangoNafsiMgawanyo wa AfrikaUpinde wa mvuaMofimuJinsiaVieleziMkoa wa RukwaChatuIdi AminMkoa wa ArushaNahauHekalu la YerusalemuHadithi🡆 More