Kupro

Kupro (pia: Kipro, Kuprosi, na hata Saiprasi kutoka Kiingereza Cyprus) ni nchi ya kisiwani upande wa mashariki wa bahari ya Mediteranea.

Kupro
Kupro
Ramani ya Kupro

Kijiografia ni sehemu ya Asia, lakini kiutamaduni na kisiasa ni sehemu ya Ulaya.

Mji mkuu ni Nikosia.

Historia

Kisiwa cha shaba

Watu waliishi huko walau kuanzia milenia ya 10 KK.

Zamani za Kale kisiwa kilikuwa chanzo cha shaba nyingi iliyopatikana katika eneo la Mediteranea ya mashariki. Jina la kikemia la shaba "kupri" linatokana na jina la kisiwa hicho.

Katika Biblia

Kisiwa kinazungumziwa na Biblia ya Kikristo, kwa namna ya pekee kuhusiana na umisionari wa Mtume Barnaba na wenzie Mtume Paulo na Marko Mwinjili kisiwani huko.

Karne za Kati

Kuanzia mwaka 649 Kupro ilishambuliwa na pengine kutawaliwa na Waarabu walioua wakazi wengi na kubomoa makanisa na miji mizima.

Chini ya Waosmani

Baada ya Wakristo kujirudishia kisiwa hicho muhimu, Waturuki Waosmani walikiteka mwaka 1570 na kuingiza Uislamu bila kufaulu kufuta dini ya awali.

Chini ya Waingereza

Mwaka 1878 Uingereza ulianza kutawala Kupro bila kuitenga rasmi na Dola la Waosmani hadi mwaka 1914.

Uhuru

Tarehe 16 Agosti 1960 Kupro ilijipatia uhuru ingawa kulikuwa na utata kati ya kubaki peke yake, kuungana na Ugiriki au kugawiwa kati ya kaskazini (Waturuki) na kusini (Wagiriki).

Baada ya uhuru

Tangu vita vya Kupro, 1974 kisiwa kimegawiwa, huku maeneo ya kaskazini yakiwa yanatawaliwa na Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini isiyotambulika kimataifa.

Pamoja na hayo, Kupro imefaulu kujiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Mei 2004.

Watu

Wakazi walio wengi hutumia lugha ya Kigiriki, wengine Kituruki, ambazo zote mbili ni lugha rasmi.

Kwa jumla hao wa kwanza ni Wakristo (72.3% za wakazi wote), wa pili ni Waislamu (25%).

Wakristo karibu wote ni Waorthodoksi; wengine ni Wakatoliki (2.9%, hasa Wamaroni), Waprotestanti (2%) na Waarmenia.

Dini ina nafasi kubwa katika maisha ya wananchi.

Tazama pia

Viungo vya nje

Kupro 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Government
    Tourism
    Official publications

33°E / 35°N 33°E / 35; 33

Nchi za Umoja wa Ulaya Kupro 
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Kupro  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kupro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Kupro  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kupro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Kupro HistoriaKupro WatuKupro Tazama piaKupro Viungo vya njeKuproBahariKiingerezaMasharikiMediteraneaNchi ya kisiwani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

HektariBendera ya KenyaUaTreniHaki za watotoTetekuwangaMuundo wa inshaOrodha ya Mashirika ya Ndege DunianiFigoUkoloniMkunduMwenge wa UhuruKenyaJinaHadithi za Mtume MuhammadViunganishiKisimaMafarisayoUzazi wa mpangoRadiSkriniArsenal FCMnyoo-matumbo MkubwaANchi za visiwaHifadhi ya NgorongoroWazigulaWanyamweziUyahudiOrodha ya Marais wa MarekaniRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniKimondo cha MboziDakuAlbert EinsteinVivumishi vya pekeeMkoa wa GeitaUsimbajiSarufiMaghaniLongitudoFananiMobutu Sese SekoRiadhaMaadiliMekatilili Wa MenzaKilimanjaro (Volkeno)Wizara za Serikali ya TanzaniaVivumishiMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaMavaziJeshiTungo kishaziMilki ya OsmaniOrodha ya Marais wa UgandaWimbo wa TaifaMaumivu ya kiunoMjasiriamaliJamhuri ya Watu wa ZanzibarLugha fasahaUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaJumuiya ya Afrika MasharikiKaswendeNembo ya TanzaniaWallah bin WallahNamba za simu TanzaniaLady Jay DeeKiunguliaNgome ya YesuAdolf HitlerMaudhui katika kazi ya kifasihiTarakilishiWahaJipuMkanda wa jeshi🡆 More