Mwezi wa Julai ni mwezi wa saba katika Kalenda ya Gregori.
Jun - Julai - Ago | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | 31 | ||||
Kalenda ya Gregori |
Jina lake limetokana na jina la Julius Caesar wa Warumi (angalia pia Kalenda ya Juliasi). Kwa asili, mwezi huo wa Julai ulikuwa mwezi wa tano katika kalenda ya Warumi, na jina lake lilikuwa Quintilis kulingana na neno la Kilatini quintus, maana yake ni "wa tano". Mwaka wa 153 KK, mwanzo wa mwaka ulitanguliza miezi miwili kutoka Machi kwenda Januari, na maana ya jina Quintilis ilipotea. Mwaka wa 44 KK, Quintilis ilibadilika kuitwa Julai (kwa Kilatini Julii).
Julai ina siku 31, na inaanza na siku ya juma sawa na mwezi wa Aprili; na katika mwaka mrefu (wenye siku 366), siku yake ya kwanza pia ni sawa na mwezi wa Januari.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Julai, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.