Togo ni nchi ya Afrika ya Magharibi inayofikia kwenye mwambao wa Ghuba ya Guinea (bahari ya Atlantiki) ikipakana na Benin upande wa mashariki, Burkina Faso kaskazini na Ghana mashariki.
Togo |
---|
Idadi ya wakazi ilikuwa zaidi ya milioni 8 u nusu mwaka 2022.
Mji mkuu ni Lome.
Togo ni nchi ndogo katika Afrika yenye km² 56,785 pekee kwa umbo la pembenne lenye urefu wa urefu wa kilometa za mraba km 550 na upana wa takriban km 130. Mwelekeo wa eneo la nchi ni kaskazini - kusini.
Humo kuna kanda zote za kijiografia za Afrika ya Magharibi kuanzia pwani yenye mchanga na misitu ya minazi kusini, vilima vya nyanda za juu katikati na savana pamoja na maeneo yabisi zaidi ya Sahel kaskazini.
Nchi ilianzishwa kama koloni la Togo ya Kijerumani katika pengo kati ya maeneo ya Uingereza na Ufaransa.
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia koloni la Kijerumani liligawiwa kati ya majirani hao kama eneo lindwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na baadaye ya Umoja wa Mataifa.
Mnamo Desemba 1956 wakazi wa Togo ya Kiingereza waliamua kwa kura kubaki na Ghana. Hivyo ni Togo ya Kifaransa pekee iliyopata uhuru mwaka 1960.
Rais wa kwanza alikuwa Sylvanus Olympio.
Nchini kuna makabila 37; kubwa zaidi ni Waewe (32%). Wazungu hawafikii 1%.
Lugha rasmi ni Kifaransa, ingawa kwa kawaida wakazi wanazungumza lugha za kikabila.
Upande wa dini, mwaka 2020 ilikadiriwa kuwa 47.8% ni Wakristo (hasa wa Kanisa Katoliki) 33% wanafuata dini asilia za Kiafrika na 18.4% ni Waislamu (hasa Wasuni).
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Togo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Togo, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.