Ufalme wa Lesotho, au Lesotho, ni nchi ndogo inayozungukwa na Afrika Kusini pande zote.
Haina pwani kwenye bahari yoyote.
Lesotho |
---|
Jina Lesotho lamaanisha eneo la Basotho (wakazi 99.7%), watu ambao wanaongea lugha ya Kisotho, ambayo ni lugha rasmi pamoja na Kiingereza. Wakati wa ukoloni ilijulikana kama Basutoland.
Sasa ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa.
Ina wakazi milioni 2 hivi.
Mji mkuu ni Maseru.
Ukweli wa kijiografia ambao wajulikana zaidi kuhusu Lesotho ni kwamba ni nchi inayozungukwa na Afrika ya Kusini, na ni nchi huru pekee duniani ambayo yote iko juu ya mita 1,000 juu ya usawa wa bahari (UB) (ft 3,281). Eneo la chini zaidi liko mita 1,400 (futi 4,593), na zaidi ya asilimia 80 za nchi ziko juu ya mita 1,800 (futi 5,906).
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.
Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
Lesotho ya sasa ilianza kupatikana mwaka 1822 chini ya chifu Moshoeshoe I aliyeungana na makabila mengine dhidi ya Shaka Zulu (1818-1828).
Baadaye nchi iliathiriwa na mahusiano na Waingereza na Makaburu wa . Koloni la Rasi (leo Afrika Kusini), yakiwemo mapigano ya mara kwa mara.
Wamisionari walioalikwa na Mfalme Moshoeshoe I walianza kuandika na kuchapa kwa lugha ya Kisotho kati ya miaka 1837 na 1855.
Mwaka 1867 nchi ikawa chini ya malkia wa Uingereza kwa jina la Basutoland lakini mwaka 1869, Waingereza waliwaachia Makaburu nusu ya eneo la Basutoland.
Uhuru ulipatikana tena mwaka 1966, na nchi ikaitwa ufalme wa Lesotho.
Kwa usimamizi wa serikali, Lesotho imegawiwa katika wilaya 10, kila moja ikiongozwa na Karani wa wilaya.
Kila wilaya ina mji unaoitwa mji wa kambi (camptown).
|
|
Wakazi kwa asilimia 90 ni Wakristo, wakigawanyika karibu sawa kati ya Wakatoliki na Waprotestanti wa madhehebu mbalimbali.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lesotho kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Lesotho, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.