Korea Kusini

Korea ya Kusini (jina rasmi: Jamhuri ya Korea) ni nchi ya Asia ya Mashariki iliyopo kusini mwa rasi ya Korea.

Korea Kusini
Korea Kusini
Ramani ya Korea ya Kusini

Upande wa kaskazini imepakana na Korea ya Kaskazini. Korea zote mbili zilikuwa nchi moja hadi mwaka 1945 chini ya utawala wa kikoloni wa Japani.

Ng'ambo ya bahari iko Uchina upande wa magharibi na Japani upande wa kusini-mashariki.

Mji mkuu, pia mji mkubwa, ni Seoul ambako karibu nusu ya wakazi wote huishi ama mjini ama katika mazingira yake. Seoul ni kati ya miji muhimu ya biashara na uchumi kimataifa.

Historia

Utamaduni wa Korea ni kati ya zile za kale zaidi duniani.

Tangu maungano ya kitaifa ya Korea yote mwaka 668 KK ilikuwa nchi moja hadi mwaka 1910 ilipofanywa koloni la Japani.

Uhuru baada ya mwaka 1945 ulifuatwa na mgawanyiko wa nchi na kuundwa kwa Korea Kusini.

Awali ilikuwa nchi maskini yenye uchumi wa kilimo, lakini iliendelea kuwa nchi ya viwanda iliyofaulu kusogea mbele na kujenga demokrasia imara.

Siku hizi imekuwa moja ya nchi tajiri ya Asiaː ina nafasi ya 13 duniani kati ya mataifa matajiri. Iko kati ya nchi kumi duniani zinazouza bidhaa nyingi nje.

Hali ya maisha ni ya juu na viwanda vyake vinatengeneza bidhaa za kisasa kabisa kama motokaa, meli, mashine, vifaa vya kompyuta na nyinginezo.

Miji

Mikoa

Kuna mikoa tisa nchini Korea Kusini, zikiwemo:

Watu

Wakazi karibu wote (99 %) ni Wakorea asili. Wachina ni 1.8 %, lakini wengi wao wana asili ya Korea.

Idadi ya watu inaelekea kupungua kutokana na uzazi kuwa wa nadra mno (watoto 9 kwa watu 1,000ǃ).

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kikorea.

Dini

Kiasili watu wa Korea walifuata dini ya jadi iliyoheshimu mapepo mbalimbali na kutoa sadaka kama njia za kuyapatanisha.

Tangu karne ya 4 Ubuddha uliingia kutoka China ukawa dini rasmi.

Ukonfusio ulifuata tangu karne ya 13.

Ukristo ulingia pia kutoka China ukaanza kukua zaidi tangu karne ya 19.

Siku hizi takriban nusu ya Wakorea wa kusini wasema hawana dini. Sehemu kubwa wanakadiriwa kuwa wafuasi wa Konfusio lakini hawajiiti "wanadini".

Ukristo ni kundi kubwa la kidini ukiwa na 29 % za Wakorea wa Kusini, wakiwemo Waprotestanti (18.3 %) na Wakatoliki (10.9 %). Wabuddha ni kama 22.8 %. Kuna pia wafuasi wachache wa dini nyingine mbalimbali.

Tazama pia

Viungo vya nje

Korea Kusini 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.

Tags:

Korea Kusini HistoriaKorea Kusini MijiKorea Kusini MikoaKorea Kusini WatuKorea Kusini Tazama piaKorea Kusini Viungo vya njeKorea KusiniAsia ya MasharikiRasi ya Korea

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

DuniaWilaya za TanzaniaLugha ya taifaOsama bin LadenNomino za wingiNgonjeraKongoshoNetiboliAdhuhuriKisaweAina za udongoTaswira katika fasihiMunguLenziVivumishi vya idadiZabibuWasabatoNdege (mnyama)MaishaNandyUongoziGridiOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaUfupishoVita ya Uingereza dhidi ya ZanzibarWamasaiTanganyika African National UnionItifakiKiimboShambaNambaHektariSintaksiKodi (ushuru)Vivumishi vya jina kwa jinaMkoa wa KilimanjaroKitenzi kikuu kisaidiziMaana ya maishaJulius NyerereOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaMimba kuharibikaHekalu la YerusalemuWizara za Serikali ya TanzaniaUmoja wa MataifaMwanaumeMpira wa miguuMatumizi ya LughaAthari ya pandemia ya Korona 2019-20 kwa mazingiraMethaliNahodhaNomino za pekeeGoogle ChromeMbadili jinsiaNafsiAmfibiaMadiniMwaka wa KanisaMlo kamiliMohammed Gulam DewjiHeshimaMgawanyo wa AfrikaMatamshiFonetikiWabunge wa Tanzania 2020Bongo FlavaMatiniJiniWanyama wa nyumbaniMamlaka ya Mapato ya TanzaniaAlfabetiWamalila🡆 More