True Jesus Church ni kanisa la kujitegemea la Ukristo wa Kiprotestanti lililo na asili huko Beijing, Uchina, mwaka 1917.
Kanisa hilo linaamini teolojia ya "Mungu Mmoja wa Kweli".
Mwenyekiti wa sasa wa TJC International Assembly aliyechaguliwa ni mhubiri Yong-Ji Lin.
Kwa sasa, kuna wanachama takriban milioni 1.5 hadi 3 katika nchi sitini na tano za mabara sita.
Idadi kubwa wako ndani ya Uchina ambako si rahisi kuhakikisha idadi kamili kwa sababu TSC ni kati ya makanisa na vikundi vya Kikristo vilivyopigwa marufuku na serikali ya nchi hiyo.
Tovuti za TJC katika nchi mbalimbali zinataja Wakristo 70,000 hadi 80,000 katika "nchi huru", wengi wao wakiwa na asili ya Kichina.
Kanisa lilianzishwa wakati wa kustawishwa kwa harakati za Kipentekoste nchini Uchina mwanzo wa karne ya 20. Harakati hizi zilianzia Marekani wakati wa mkutano wa kwanza wa Kipentekoste katika Azusa Street Revival huko Los Angeles iliyoongozwa na William J. Seymour miaka [1906]]-1908.
Toka huko tapo hilo lilienea hadi Uchina.
Kulikuwepo moja ya nyumba tatu za Kichina zilizotengenezwa kabla ya Chama cha Kikomunisti cha Uchina kuchukua mamlaka mwaka 1949.
Kanisa lina lengo la kuhubiri injili kwa kila nchi kabla ya kurejea kwa Yesu Kristo.
Tangu mwaka 2002 lilianza kuwasiliana na kikundi cha kikristo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kilichojiunga nalo mnamo mwaka 2004.
Wanajieleza kwamba Yesu Kristo alianzisha Kanisa moja la kimitume lililopeleka Injili katika nchi mbalimbali. Lakini Kanisa hilo likavurugika na kupatwa na imani potovu na uzushi hadi mwaka 1917 Mungu alipoamua kulifufua kwa nguvu ya Roho Mtakatifu na ndio mwanzo wa TJC.
Kati ya imani nyingine za pekee ni hizi zifuatazo:
Mafundisho mengine yanafanana na yale ya Wapentekoste, kama vile kusema kwa lugha za roho au kubatizwa kwa jina la Yesu kwa kuzamishwa chini ya maji, tena maji ya kutiririka.
Ingefaa ueleweke ukweli wa msimamo wa TJC kulingana na Biblia wanapodai kwa miaka mia kadhaa duniani halikuwepo tena Kanisa la kweli, wakati Yesu aliahidi, "Nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:20). Tena "Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda" (Mathayo 16:18).
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu True Jesus Church kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article True Jesus Church, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.