Bahari Nyeusi

Bahari Nyeusi ni bahari ya pembeni ya Mediteranea inayozungukwa na nchi kavu pande zote iliyoko kati ya Ulaya ya Mashariki na Asia ya Magharibi.

Imeunganishwa na Bahari ya Mediteranea kwa njia ya Bahari ya Marmara pamoja na milango ya bahari ya Bosporus na Dardaneli. Ina eneo la takriban 424,000 km² na kina hadi 2,244 m.

Bahari Nyeusi
Ramani ya Bahari Nyeusi
Bahari Nyeusi
Bahari Nyeusi inavyoonekana kutoka angani (NASA)

Nchi zinazopakana ni Uturuki, Bulgaria, Romania, Ukraine, Urusi na Georgia. Rasi ya Krim ni sehemu ya kujitawala ya Ukraine.

Miji muhimu mwambaoni ni: Istanbul, Burgas, Varna, Constanţa, Yalta, Odessa, Sevastopol, Kerch, Novorossiysk, Sochi, Sukhumi, Poti, Batumi, Trabzon, Samsun na Zonguldak.

Jina

Katika lugha zote za kisasa bahari inaitwa "bahari nyeusi": Kigiriki Μαύρη θάλασσα, Kibulgaria cherno more (Черно море), Kigeorgia shavi zghva (შავი ზღვა), Kiromania Marea Neagră, Kirusi chyornoye more (Чёрное море), Kituruki Karadeniz, Kiukraine chorne more (Чорне море). Jina hili limepatikana kwa hakika tangu karne ya 13 lakini asili yake haijulikani.

Wagiriki na Waroma wa Kale waliita Euxeinos Pontos (Εὔξεινος Πόντος) au "Bahari ya ukarimu".

Bahari Nyeusi  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari Nyeusi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Asia ya MagharibiBahari ya MarmaraBahari ya pembeniBosporusDardaneliMediteraneaMlango wa bahariUlaya ya Mashariki

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)SiasaBendera ya ZanzibarMfumo wa JuaShomari KapombeNjiwaMwakaKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaHifadhi ya mazingiraBahari ya HindiKenyaPemba (kisiwa)AdhuhuriMitume wa YesuMwanaumeHistoria ya WasanguVitendawiliKilimanjaro (Volkeno)Nomino za wingiOrodha ya Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoMandhariVitenzi vishiriki vipungufuBunge la TanzaniaFalsafaHistoria ya WapareOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoMgawanyo wa AfrikaMagimbiWizara za Serikali ya TanzaniaMagadi (kemikali)Ugonjwa wa kuambukizaEe Mungu Nguvu YetuHektariCAFNge (kundinyota)DhahabuInjili ya MathayoKalenda ya GregoriDini nchini TanzaniaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaJeshiSaratani ya mapafu26 MachiNg'ombeTarbiaUkooUandishi wa ripotiUNICEFSteve MweusiUandishi wa barua ya simuPijini na krioliHaitiMexikoJumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta dunianiEdward Ngoyai LowassaBukayo SakaUhuru wa TanganyikaAmfibiaChuma barani AfrikaWikipediaKatekisimu ya Kanisa KatolikiTelevisheniOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaUkristoMpira wa kikapuHistoria ya KanisaWaluguruWamandinkaKimondo cha MboziWajitaUtoaji mimbaKipindi cha PasakaJuaUfahamu🡆 More