Usufii

Usufii (kar.

صوفی sufi) pia tasawuf (kar. تصوف ) au Uislamu wa Kisufii ni tawi la Uislamu linalotafuta maarifa ya moyoni kuhusu ya Mungu na imani.

Usufii
Sufi (dervish) jinsi anavyocheza mbele ya msikiti huko Omdurman, Sudan

Wafuasi wa mwelekeo huu wanaweza kuitwa Sufii, Dervish au Fakir.

Imani

Wasufii wanaamini ya kwamba inawezekana kumkaribia Mungu katika maisha ya sasa kabla ya kifo wakielekea kuungana na nuru au roho ya Allah iwezekanavyo.

Wanakazia kutawala fikra na tamaa za kimwili na kuondoa kila kitu ndani ya nafsi kisicholingana na Mungu. Kwa njia hii walimu wao wanafundisha kuna uwezekano kuachana na nafsi kabisa na kusikia umoja na Mungu.

Wasufii wengi hukazia upendo wa Mungu na upendo kwa Mungu.

Kwa kukaribia shabaha hii Wasufii wengine wanafundisha maisha ya kuachana na dunia na tamaa na mambo yake yote. Hapo wanaweza kufanana na watawa katika dini nyingine kama vile Wakristo au Wahindu ingawa hawajui amri ya useja au kutooa.

Tarika

Wasufii wengi wameungana katika jumuiya mbalimbali zinazoitwa "tarika" (kar. طريقة - "njia") na jumuiya hizi hufuata maagizo wa kiongozi (mara nyingi mwenye cheo cha sheikh) aliyeiunda.

Wanakutana kwa mazoezi ya kiroho na haya ni pamoja na dhikr (kumbukumbu kwa Mungu kwa njia ya kurudiarudia jina Allah au majina yake mengine), uimbaji na kucheza. Sehemu ya Wasufii wanatumia aina ya kucheza ambako kila mshiriki anazunguka kiduara.

Kati ya jumuiya makubwa ya Wasufi ni

  • Qadiri au Qadiriyya;
  • Chishti au Chishtiyya;
  • Suhrawardi au Suhrawardiyya;
  • Naqshbandi au Naqshbandiyya;
  • Mevlevi au Mevleviyya;


Wasufi mashuhuri

Kati ya Wasufii waliokuwa mashuhuri ni wafuatao :

  • Uwais al-Qarni
  • Dhul Nun Misri
  • Junaid of Baghdad
  • Rabia Basri
  • Hasan Basri
  • Bayazid Bastami
  • Ibn ul-Arabi
  • Al-Ghazali
  • Abd al-Qadir al-Gillani
  • Shahab-ud-din Suhrawardi
  • Farid-ud-din Attar
  • Baha-ud-din Naqshband
  • Ali al-Hajvery
  • Jalal-ud-din Rumi
  • Moin-ud-din Chishti
  • Farid-ud-din Ganj Shakar
  • Nizam-ud-din Auliya
  • Lal Shahbaz Qalandar
  • Hakim Omar Khayyam

Usufi na Uislamu rasmi

Mazoezi ya Wasufi hazikubaliki na sehemu za Waislamu wengine. Wasufi wameshtakiwa kutembea nje ya Uislamu.

Hasa mielekeo makali kama Wahabiya au Salafiya imepinga Wasufii na kuwashambulia pale walipo na nguvu au mamlaka. Siku hizi nyumba na mikutano ya Wasufi zimeshambuliwa hasa nchini Pakistan.. Kiongozi wao Riaz Ahmed Gohar Shahi na vitabu vyake vimepigwa marufuku na wafuasi wanaojulikana wanakamatwa. .

Nchini Saudia wataalamu wa kidini wa serikali walitangaza Usufii kuwa shirk lakini miaka ya nyumba kuna taarifa ya nafasi kubwa zaidi kwa wafuasi wa Usufii kuwa na mikutano.

Nchini Uajemi (Iran) serikali inajaribu pia kuwafuata Wasufii kwa kufunga nyumba zao. .

Kinyume chake mkutano wa kimataifa wa wataalamu waislamu nchini Jordan ilitangaza mwaka 2005 kuwa Usufi ni tawi halali la Uislamu. .

Kujisomea

  • Abu-Nasr, J (2007) Muslim Communities of Grace:Sufi Brotherhoods in Islam London;
  • Burckhardt, T (1963) An Introduction to Sufi Doctrine Lahore;
  • Godlas, A (2000) Sufism's Many Paths U of Georgia Press;
  • Shah, Idries (1971) The Sufis New York;
  • Schimmel, A (1983) Mystical Dimensions of Islam Chapel Hill: U of North Carolina Press;
  • Smoley, Richard & Kinney, Jay. 2006. Hidden wisdom: a guide to the western inner traditions. 2nd ed; Wheaton, Illinois: Quest Books. ISBN 978-0-8356-0844-2 (Chapter 10 deals with Sufism in the West)

Marejeo

Tags:

Usufii ImaniUsufii TarikaUsufii Wasufi mashuhuriUsufii Usufi na Uislamu rasmiUsufii KujisomeaUsufii MarejeoUsufiiKar.Uislamu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

20 ApriliWahayaKutoka (Biblia)Mkoa wa ArushaSentensiHarusiVita ya Maji MajiVivumishi vya sifaMkoa wa ShinyangaOrodha ya Marais wa TanzaniaNuktambiliJumapiliJérémy DokuTeknolojiaMtandao wa kompyutaMkoa wa IringaJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoKukosa usingiziWairaqwWaamuzi (Biblia)WagogoMuda sanifu wa duniaMadhara ya kuvuta sigaraAKitenziWakingaVasco da GamaVivumishi vya urejeshiMpungaDiamond PlatnumzArsenal FCTitanicMapenzi ya jinsia mojaUNICEFUmaskiniKiini cha atomuRaiaIntanetiManchester CityTamthiliaTarakilishiDini asilia za KiafrikaAmri KumiDivaiPaneli ya solaMguuGesi asiliaChakulaRuge MutahabaVihisishiViwakilishi vya pekeeDubaiWaheheKidole cha kati cha kandoMwanza (mji)Hussein KaziSeduce MeHaki za binadamuVivumishi vya kumilikiViungo vinavyosafisha mwiliJeneraliJipuMsamahaPentekosteDhahabuKunguru🡆 More