Jiji ni mji mkubwa.
Kuna tofauti kati ya nchi na nchi wakati wa kueleza ni sifa gani pamoja na ukubwa gani vinavyofanya mji kuwa mji mkubwa au jiji.
Kimataifa kulikuwa na makubaliano kwenye mkutano wa kimataifa wa takwimu ya mwaka 1887 ya kuhesabu kila mji wenye wakazi zaidi ya 100,000 kama "mji mkubwa", miji kati ya wakazi 20,000 na 100,000 kama miji ya wastani na ile kati ya wakazi 5,000 na 20,000 kama miji midogo. Kufuatana na hesabu hiyo kulikuwa na miji mikubwa 1,700 duniani mnamo mwaka 2002.
Nchini Tanzania ni Dar es Salaam pamoja na Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Tanga, inayoitwa "jiji"; nchini Kenya ni Nairobi pamoja na Mombasa na Kisumu. Kati ya miji hiyo ni Nairobi na Dar es Salaam pekee yenye wakazi zaidi ya milioni mbili.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Jiji, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.