Georgia

Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Georgia (maana)

Georgia
Georgia
Ramani ya Georgia

Georgia (kwa Kigeorgia: საქართველო "Sakartvelo") ni nchi ya Kaukazi kati ya Ulaya na Asia kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi.

Imepakana na Urusi, Uturuki, Armenia na Azerbaijan.

Georgia ina wakazi milioni 3.7. Zaidi ya milioni 1 hukaa mjini Tbilisi ambao ndio mji mkuu wa nchi.

Jiografia

Georgia ni nchi ya milima ya Kaukazi inayofikia kimo cha mita 5,068. Kati ya safu mbili za milima kuna tambarare ya Kolkhis.

Upande wa magharibi unafaidika zaidi na Bahari Nyeusi, hivyo una hali ya hewa safi na mvua nyingi inayofaa kwa kilimo hasa cha mizabibu.

Historia

Georgia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti lakini imekuwa nchi huru tangu 1991.

Maeneo ya Abkhazia na Ossetia ya Kusini yamedai uhuru pia na kwa sasa hayapo chini ya serikali kuu, lakini hayatambuliki kimataifa.

Utamaduni

Wakazi walio wengi (71%) huzungumza lugha ya Kigeorgia lakini kuna vikundi vya wazungumzaji wa Kirusi (9%), Kiarmenia (7%), Kiazeri (6%) na lugha nyingine.

Wageorgia wengi ni Wakristo wanaofuata Kanisa la Kiorthodoksi la Georgia (83.9%). Kuna pia wafuasi wa Kanisa la Kitume la Armenia (3.9%) na Wakatoliki (0.8%). Waislamu ni 9.9%, wakati Wayahudi wanazidi kuhama.

Watu maarufu

Mgeorgia anayejulikana zaidi duniani alikuwa Josef Stalin, mtawala wa Urusi wakati wa Ukomunisti.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Georgia 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Serikali
    Taarifa za jumla
    News media
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Georgia  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Georgia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Georgia  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Georgia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Georgia JiografiaGeorgia HistoriaGeorgia UtamaduniGeorgia Watu maarufuGeorgia Tazama piaGeorgia TanbihiGeorgia Viungo vya njeGeorgiaGeorgia (maana)

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MaghaniTamthiliaUgonjwaVidonge vya majiraMaambukizi nyemeleziNimoniaOrodha ya makabila ya TanzaniaViwakilishi vya kumilikiJuxKipindupinduKajala MasanjaMnyoo-matumbo MkubwaKengeRamaniMkoa wa KilimanjaroUkristo barani AfrikaHotubaSteven KanumbaWapareMgawanyo wa AfrikaMitume na Manabii katika UislamuIlemelaKomaMnyamaUkristoMkoa wa TaboraChupaOrodha ya Marais wa MarekaniUlemavuMisemoLugha ya taifaUtandawaziAngahewa23 ApriliNgome ya YesuOrodha ya majimbo ya MarekaniLugha fasahaAfrika Mashariki 1800-1845PumuSitiariAina za manenoMikoa ya TanzaniaMfumo wa upumuajiMaskiniUfupishoKamusi ya Kiswahili sanifuMavaziUtapiamloUtamaduniVivumishi vya kuoneshaNomino za kawaidaHaki za watotoMillard AyoUlayaMfumo wa mzunguko wa damuDemokrasiaJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaKenyaMtemi MiramboBumbuliMtandao pepe binafsiOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaMashariki ya KatiFananiMnazi (mti)Magonjwa ya kukuBiashara ya watumwaMkoa wa Dar es SalaamMuundoUshairiKiimboMungu ibariki AfrikaVivumishi vya sifaMaumivu ya kiunoAkili ya binadamu🡆 More