Albania

Jamhuri ya Albania ni nchi ya Ulaya Kusini Mashariki.

Imepakana na Montenegro, Kosovo, Masedonia Kaskazini na Ugiriki. Upande wa magharibi kuna pwani ya ghuba ya Adria ya bahari ya Mediteranea.

Albania

Albania ni kati ya nchi zinazoendelea na imeomba kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Mji mkuu ni Tirana (wakazi 418,495).

Historia

Historia ya kale

Albania ilikaliwa na makabila mbalimbali ya Wailiriko, Wathraki na ya Wagiriki.

Katika karne ya 3 KK eneo lilitekwa na Dola la Roma na kufanywa sehemu ya majimbo ya Dalmatia, Masedonia na Iliriko.

Karne za Kati

Mwaka 1190 ndani ya Dola la Roma Mashariki ulitokea ufalme mdogo wa Arbër kwa juhudi za archon Progon huko Krujë.

Mwishoni mwa karne ya 13 Charles wa Anjou aliwanyang'anya Wabizanti eneo hilo na kuanzisha Ufalme wa Albania kutoka Durrës hadi Butrint.

Katikati ya karne ya 15 nchi ilitekwa na Waosmani.

Historia ya kisasa

Albania ya sasa ilitokea mwaka 1912, baada ya Waosmani kushindwa katika vita vya Balkani.

Ufalme wa Albania ulitekwa na Italia ya Benito Mussolini mwaka 1939 hadi 1943, ulipowekwa na Ujerumani wa Adolf Hitler chini yake.

Baada ya nchi hizo mbili kushindwa vitani, nchi ikaongozwa na Enver Hoxha ikijitenga zaidi na zaidi na dunia nzima.

Kati ya miaka 1945 na 1990 ilipotawaliwa na chama cha Kikomunisti Albania ilitangaza kuwa nchi ya kwanza ya kiatheisti na kupiga marufuku kila aina ya dini.

Kutokana na mapinduzi ya mwaka 1991 Jamhuri ya Kisoshalisti iliiachia nafasi jamhuri ya nne.

Kwa sasa Albania ni kati ya nchi maskini zaidi za Ulaya na wananchi wengi (walau 900,000) wamehamia Ugiriki, Italia, Marekani n.k.

Watu

Wamebaki wakazi 2,876,591 (2017). Zaidi ya 98% za wakazi hutumia lahaja za Kialbania ambacho ni lugha ya pekee kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Lakini wengi wanazungumza pia Kigiriki au lugha nyingine.

Kati ya miaka 1945 na 1990 ilitawaliwa na chama cha Kikomunisti iliyotangaza Albania kuwa nchi ya kwanza ya kiatheisti iliyopiga marufuku kila aina ya dini. Hata hivyo, baada ya uhuru kupatikana tena, 39% za wakazi anajali sana imani fulani. Katika sensa ya mwaka 2011, 58.79% walijitambulisha kama Waislamu (hasa Wasuni) na 17.06% Wakristo (wakiwemo 10.03% Wakatoliki na 6.75% Waorthodoksi). Wakanamungu walikuwa 2.5% tu.

Tazama pia

Viungo vya nje

Albania 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Albania  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Albania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Albania HistoriaAlbania WatuAlbania Tazama piaAlbania Viungo vya njeAlbaniaAdriaBahariGhubaKosovoKusiniMagharibiMasedonia KaskaziniMasharikiMediteraneaMontenegroPwaniUgirikiUlaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Jumuiya ya Afrika MasharikiZakayoMsamiatiMillard AyoZana za kilimoReptiliaUshairiUNICEFNamba za simu TanzaniaKampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya MasharikiMweziNusuirabuUlumbiMitume na Manabii katika UislamuMwanzo (Biblia)KonsonantiHistoria ya ZanzibarTungo kishaziNambaUajemiWimboOrodha ya viongoziMlo kamiliMalariaOrodha ya Marais wa MarekaniKupatwa kwa JuaMbuMkanda wa jeshiJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaMhusika (fasihi)StashahadaVita ya Maji MajiHistoria ya KiswahiliFalsafaWanyamaporiKitenziOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuMatumizi ya LughaSteven KanumbaMkoa wa KilimanjaroNomino za dhahaniaTetemeko la ardhiThamaniPandaUbuddhaMshale (kundinyota)Jakaya KikweteUlayaSoga (hadithi)Bendera ya KenyaDubuUfeministiHafidh AmeirMaana ya maishaAlama ya uakifishajiKiarabuKupatwa kwa MweziVielezi vya idadiViwakilishi vya kuulizaBomu la nyukliaNzigeMashariki ya KatiJoseph Leonard HauleDawatiYesuUhindiSarufiWenguEe Mungu Nguvu YetuKilimanjaro (volkeno)Huzuni🡆 More