Kipepeo

Familia za juu 2, familia 7:

Kipepeo
Papilio antimachus, kipepeo mkubwa kabisa wa Afrika
Papilio antimachus, kipepeo mkubwa kabisa wa Afrika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Lepidoptera (Nondo na Vipepeo)
Nusuoda: Glossata (Vipepeo wenye ulimi mrefu)
Fabricius, 1775
Ngazi za chini

  • Hedyloidea Scoble, 1986
    • Hedylidae Guénée, 1857
  • Papilionoidea Latreille, 1802
    • Hesperiidae Latreille, 1809
    • Lycaenidae Leach, 1815
    • Nymphalidae Rafinesque, 1815
    • Papilionidae Latreille, 1802
    • Pieridae Swainson, 1820
    • Riodinidae Grote, 1895

Vipepeo ni wadumili (hali ya mwisho ya metamofosisi) wa wadudu wa oda ya Lepidoptera.

Kipepeo
Kipepeo aina ya (Gonepteryx rhamni) akiruka

Jinsi ilivyo kwa wadudu wengi maisha ya kipepeo huanza kama yai. Anatoka kwenye yai kwa umbo la kiwavi. Baada ya miambuo minne kiwavi huwa bundo. Ndani ya bundo hugeuka kuwa kipepeo anayetoka na kutaga mayai tena. Mzunguko huu kwa jumla unaitwa metamofosisi.

Vipepeo huishi kwa muda mfupi. Hula kiowevu pekee, hasa cha mbochi wa maua.

Kipepeo
Cairn's birdwing

Utangulizi

Kipepeo 
Papilio xuthus

Vipepeo wa kweli ni wadudu wa nusuoda Glossata. Wana wengine wa Lepidoptera huitwa nondo. Kama ilivyo kwa wadudu wengi mzunguko wa maisha wa vipepeo huwa na sehemu nne: yai, lava (kiwavi), bundo na mdumili (imago). Spishi nyingi zaidi huruka wakati wa mchana. Rangi zao za kupendeza na miruko yao ya mbwembwe hufanya kuangalia vipepeo kuwa miongoni mwa tabia za kupendeza kwa baadhi ya watu.

Vipepeo wengi kiasili wamepitia mabadiliko makubwa. Wengine wametoka na na mabadiliko kutoka kwa wadudu kama vile mchwa. Vipepeo ni muhimu sana kwa kusaidia uchavushaji kwa binadamu, sababu zinapelekea mharibifu wa mazao hasa katika hatua ya lava ya ukuaji nao kitamaduni, vipepeo ni motifu maarufu katika sanaa ya maandishi na maonesho.

Vipepeo na nondo

Kipepeo 
Kipepeo akiwa kwenye nyasi

Spishi nyingi zaidi za Lepidoptera ni nondo. Tofauti kati ya nondo na vipepeo ni kama ifuatavyo. Vipapasio vya vipepeo ni kama nyuzi zenye kinundu mwishoni kwao. Nondo wana vipapasio vyenye maumbo mbalimbali lakini abadani nyuzi zenye kinundu. Juu ya hayo takriban nondo wote hukiakia wakati wa usiku na vipepeo hukiakia wakati wa mchana.

Mzunguko wa maisha

Kipepeo 
Common buckeyes wakijamiiana

Ni imani iliyoweleka kwamba vipepeo maisha kwa muda mdogo sana. Hata hivyo, kulingana na aina zao, vipepeo kisha kuishi kwa wiki moja mpaka hata takriban mwaka mmoja.

Vipepeo wana kizazi kimoja au vizazi kadhaa kwa mwaka. Hutofautiana kutoka sehemu moja mpaka nyingine, huku maeneo ya tropiki yakionekana kuchochea uzazi kwa kiasi kikubwa.

Mayai

Kipepeo 
Yai la Ariadne merione

Mayai ya vipepeo huwa na gamba gumu liitwalo korioni (chorion). Gamba hili limezungukwa na nta inayozuia yai lisikauke kabla ya lava hajakua vizuri. Kila yai huwa na tunau dogo, kwa ajili ya kuruhusu manii kuingia na kurutubiha yai. Mayai ya vipepeo na nondo hutofautiana sana kwa ukubwa kwenye spishi zao, lakini yote huwa ya miduara au dharadufu.

Mayai ya kipepeo hushikizwa kwenye majani kwa gunai maalumu inayokauka haraka. Inavyokauka husinyaa, hivyo kuharibu kidogo umbo la yai. Gundi hii huonekana kuwa urahisi chini ya yai. Asili ya gundi hii haijafahamika bado, hivyo utatiti unatakiwa kufanyika.

Mayai mava zote hutasuwa kwenye mimea. Kila spishi ya kipepeo huwa na mimea yake inayopendelea kutaga mayai yake humo, huku baadhi yao wakiwa na uwezo wa kutaga kwenye mimea mingi zaidi.

Mayai hudumu kwa siku kadhaa, lakini mayai mengi hutagwa msimu wa kipupwe na kuanguliwa nyakati za kuchipua. Vipepeo wengine hutaga mayai yao nyakati za kuchupua na kunyaangua msimu wa kiangazi.

Kiwavi

Kipepeo 
Viwavi wa common buckeye

Lava wa vipepeo au viwavi hula majani kwa wingi, na hutumia muda wao mwingi wa siku wakitafuta chakula japokuwa asilimia kuowa ya viwavi hula nyasi (majani), wachache hula wadudu. Baadhi ya viwavi huishi maisha ya kutesemeana na sisimizi. Huwasiliana na sisimizi kwa kutumia mitikisiko maalumu na kemikali. Sisimizi hutoa ulinzi kwa lava hawa ambao nao huwapatia mchwa utamuu wa asali.

Viwavi wengine pia wana uwezo wa kuzitokeza sehemu za vichwa vyao na kuonekana kama nyoka. Pia wana madoa kama macho ya uongo kuongezea muonekano huo. Pia, huwa na uwezo wa kutoa kemikali fulani na kuitumia kama ulinzi.

Bundo

Kipepeo 
Bundo

Kiwavi anapokuwa na kukamilika, homoni kadhaa huanza kuzalishwa wakati huu, kiwavi huacha kula na kuanza kutafuta sehemu ya kutulia, na mara nyingi huwa chini ya majani. Hatimaye kiwavi hubadirika na kuwa bundo, baada ya kuambua ngozi yake kwa mara ya mwisho. Bundo kwa kawaida huwa hajongei, isipokuwa huweza kujitikisa/kujinyonga ny’onga na kutoa milio kadhaa kuwatishia madui.

Baadae bundo hukua na kupitia mabadiliko katika mfumo wa metamofosisi na kuwa kipepeo kamili.

Mdumili

Kipepeo 
Uso wa kipepeo

Katika hatua hii kipepeo huitwa mdumili. Jinsi yake pia hutambulika kwa mara ya kwanza. Huwana mbawa za mbele na nyuma, hukuza mbele zikiwa hazijajishikiza pamoja. Huwa na miguu sita. Kisha kutoka nje mara ya kwanza, vipepeo huanza kujifunza kuvuka, nani muda huu ambapo huwa hatari sana kwani huweza vamiwa na maadui. Zoezi hili huchukua saa 1 mpaka 3.

Maumbile

Kipepeo 
bawa la kipepeo, aina ya Inachis io, likiwa na rangi tofauti tofauti

Vipepeo huwa na mabawa manne, bawa la mbele na nyuma kwa upande na kuliana kushota mwili wao umegawanyika katika sehemu kuu tatu, kichwa, kifua, na fumbatio. Wana vipapasio viwili, macho ya kampaundi na ulimi (mdomo) maalumu, proboscis.

Tabia

Vipepeo hujilisha kwa mbochi wa maua. Wengine hujipatia virutubisho kutoka kwenye mbelewele, matunda yaliyooza, utomvu wa miti, kinyesi cha wanyama (20), miili iliyooza (21), madini yaliyozama mchangani na kwenye taka.

Vipepeo ni wachavushaji mahiri, na huweza kuleeba mbelewele kwa umbali mrefu, hata kilomita moja.

Picha

Viungo vya nje

Kipepeo 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

Kipepeo UtanguliziKipepeo Vipepeo na nondoKipepeo Mzunguko wa maishaKipepeo MaumbileKipepeo TabiaKipepeo PichaKipepeo Viungo vya njeKipepeo

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

ReptiliaPijini na krioliMahakama ya TanzaniaFalme za KiarabuMsongolaTafsiriMkondo wa umemeUbepariShambaOrodha ya volkeno nchini TanzaniaAzimio la Kimataifa juu ya Haki za BinadamuSitiariLionel MessiUkabailaSerikaliVidonge vya majiraUchimbaji wa madini nchini TanzaniaMitume wa YesuKupatwa kwa JuaMtotoSaratani ya mlango wa kizaziMohammed Gulam DewjiKitenzi kikuu kisaidiziFigoMandhariMajigamboMusaVivumishi ya kuulizaTeknolojiaShengMkutano wa Berlin wa 1885Salim KikekeIsimuOrodha ya Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPaul MakondaUfupishoSexMazoezi ya mwiliLigi Kuu Tanzania BaraDodoma MakuluKinjikitile NgwaleKadi ya adhabuKipindupinduWaheheViunganishiWanyama wa nyumbaniMaishaPaka (maana)MazingiraKaswendeChakulaHistoria ya IranMkoa wa MwanzaKibodiBiasharaHekimaMhusika (fasihi)Kupatwa kwa MweziVivumishi vya sifaKitomeoTanganyikaOrodha ya nchi kufuatana na wakaziMagonjwa ya machoHurafaJoseph Sinde WariobaMweziSteven KanumbaUmoja wa MataifaMachweoUkwapi na utaoWilaya ya MboziUkanda wa GazaMatamshiMkoa wa Songwe🡆 More