Praseodimi ni elementi ya kikemia yenye alama Pr kwenye jedwali la elementi.
Inayo namba atomia 59 ambayo inamaanisha ina protoni 59 ndani ya atomu. Ni metali laini yenye rangi ya kifedha-kijivu, chumvi zake ni njano-kijani. Huhesabiwa kati ya Lanthanidi na metali za ardhi adimu.
Praseodimi | |
---|---|
Praseodimi (ikitunzwa ndani ya gesi ya Arigoni) | |
Jina la Elementi | Praseodimi |
Alama | Pr |
Namba atomia | 59 |
Mfululizo safu | Lanthanidi |
Uzani atomia | 140.907 |
Valensi | 2, 8, 18, 21, 8, 2 |
Densiti | 6.475 g/cm3 |
Kiwango cha kuyeyuka | 1208 K (935 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 3403 K (3130 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 5,2 ppm |
Hali maada | mango |
Inachanganywa na magnesi kutengeneza aloi thabiti kwa ajili ya matumizi ndani za injini za eropleni. Inaweza pia kutumiwa kutia rangi ya kijani kibichi kwenye vioo.
Praseodimi ilitengwa kwanza na madini mengine mnamo 1885 na mwanakemia wa Austria Carl Auer von Welsbach. Inapatikana katika mchanga, unaoitwa mchanga wa monaziti, huko Marekani (Florida, Kalifornia), Uhindi, na Brazil.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Praseodimi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Praseodimi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.