Shaka Samvat

Shaka Samvat ni kalenda rasmi ya kitaifa nchini Uhindi inayotumiwa huko pamoja na kalenda ya Gregori.

Historia ya Kalenda hii

Kalenda ilianzishwa mwaka 1957 baada ya uhuru wa Uhindi kwa lengo la kuunda kalenda ya kitaifa inayosaidia kuunganisha nchi hii kubwa. Kalenda ilitungwa na kamati iliyochungulia zaidi ya kalenda 30 tofauti zilizowahi kutumiwa katika sehemu na tamaduni mbalimbali za Uhindini.

Ni kalenda ya jua na muundo wake unafanana na kalenda ya Kiajemi jinsi inavyotumiwa nchini Iran.

Hesabu ya miaka

Hesabu ya miaka inaanza mwaka 78 BK. Kwa hiyo mwaka 2014 katika hesabu ya Gregori unalingana na mwaka 1936–1937 wa Shaka Samvat.

Muundo wa Kalenda

Mwaka huwa na siku 365 na kugawiwa kwa miezi 12. Kila mwaka wa nne ni mwaka mrefu wa siku 366. Miezi ya kwanza huwa na siku 31, mengine siku 30. Mwezi wa kwanza (Chaitra) una siku 30 ila katika mwaka mrefu siku 31.

Mwaka huanza Machi 22 wa kalenda ya Gregori ambayo ni siku ya usawa wa mchana na usiku.

Mwezi Idadi ya siku Siku ya kwanza (kuf. na Kalenda ya Gregori)
1 Chaitra 30/31 Machi 22*
2 Vaisakha 31 Aprili 21
3 Jyaistha 31 Mei 22
4 Asadha 31 Juni 22
5 Sravana 31 Julai 23
6 Bhadra 31 Agosti 23
7 Asvina 30 Septemba 23
8 Kartika 30 Oktoba 23
9 Margashirsh (Agrahayana) 30 Novemba 22
10 Pausa 30 Desemba 22
11 Magha 30 Januari 21
12 Phalguna 30 Februari 20

Marejeo

Viungo vya Nje

Tags:

Shaka Samvat Historia ya Kalenda hiiShaka Samvat Hesabu ya miakaShaka Samvat Muundo wa KalendaShaka Samvat MarejeoShaka Samvat Viungo vya NjeShaka SamvatKalendaKalenda ya GregoriUhindi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

AngahewaMofimuFasihi andishiMethaliChristina ShushoDhima ya fasihi katika maishaMapenzi ya jinsia mojaNelson MandelaNigeriaLava Lava (mwimbaji)Amina ChifupaMartin LutherShairiWaluguruUaKaaMitume na Manabii katika UislamuMbadili jinsiaMkoa wa KataviApril JacksonSan Jose, CaliforniaUkoloniUainishaji wa kisayansiVita ya AbushiriMkoa wa LindiLigi ya Mabingwa AfrikaMaradhi ya zinaaMaishaHadhiraMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaLugha za KibantuMkoa wa Dar es SalaamMalengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifaAsidiHuduma ya ujumbe mfupiKataSimba S.C.HakiAgano JipyaNamba za simu TanzaniaKiongoziAmfibiaMapambano ya uhuru TanganyikaAli Hassan MwinyiElibariki Emmanuel KinguNabii IsayaAfrika ya Mashariki ya KijerumaniSoga (hadithi)Lil WayneKongoshoBloguWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiBunge la TanzaniaHerufi za KiarabuTanzaniaMwanga wa JuaUgonjwaUmoja wa AfrikaWiki FoundationWachaggaSalaNungununguWilaya za TanzaniaVita Kuu ya Kwanza ya DuniaKadi ya adhabuFani (fasihi)UnyagoPunyetoKipepeoRuge MutahabaBenjamin MkapaViwakilishi vya urejeshiKichochoNzigeOrodha ya Marais wa UgandaSexInsha ya wasifu🡆 More