Chad, kirasmi Jamhuri ya Chad (pia: Chadi), ni nchi huru iliyoko Afrika ya Kati.
Imepakana na Libya, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamerun, Nigeria na Niger.
Jamhuri ya Chad | |
---|---|
جمهورية تشاد (Kiarabu) République du Tchad (Kifaransa) | |
Kaulimbiu ya taifa: Unité, Travail, Progrès (Kifaransa) الاتحاد، العمل، التقدم (Kiarabu) "Umoja, Kazi, Maendeleo" | |
Wimbo wa taifa: La Tchadienne (Kifaransa) نشيد تشاد الوطني (Kiarabu) "Wimbo wa Chad" | |
Mahali pa Chad | |
Ramani ya Chad | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | N'Djamena |
Lugha rasmi | Kiarabu Kifaransa |
Makabila (asilimia) | 26.6 Wasara 12.9 Waarabu 8.5 Wakanembu 7.2 Wamasalit 6.9 Watebu 4.8 Wamasana 3.7 Wabidiyo 3.7 Wabilala 3.0 Wamaba 2.6 Wadaju 2.5 Wamundang 2.4 Wagabri 2.4 Wazaghawa 2.1 Wafulani 2.0 Watupuri 1.6 Watama 1.4 Wakaro 1.3 Wabagirmi 1.0 Wamasmaje 2.6 Wachad wengine 0.7 Wageni |
Dini (asilimia) | 55.1 Waislamu 41.1 Wakristo 2.4 Wakanamungu 1.3 dini asilia 0.1 wengine |
Serikali | Jamhuri yenye baraza la majeshi |
• Rais wa muda • Makamu wa Rais • Waziri Mkuu | Mahamat Déby Djimadoum Tiraina Succès Masra |
Eneo | |
• Eneo la jumla | km2 1 284 000 |
• Maji (asilimia) | 1.9 |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 18 523 165 |
Pato la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 12.596 |
• Kwa kila mtu | USD 702 |
Pato halisi la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 32.375 |
• Kwa kila mtu | USD 1 806 |
Maendeleo (2022) | 0.394 - duni |
Sehemu kubwa ya eneo lake ni jangwa na nchi yabisi. Kusini kuna kanda lenye hali ya hewa ya kitropiki, lakini ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo ni asilimia 3 tu za eneo lake lote .
Kaskazini kuna milima ya Tibesti.
Katikati liko beseni la ziwa Chad lililokuwa kati ya maziwa makubwa kabisa duniani lakini limepungua sana, hasa mwishoni mwa karne ya 20.
Katika milenia ya 7 KK kulikuwa na watu wengi sana katika beseni hiyo.
Katika historia kabla ya ukoloni watu wa kaskazini waliwafanyia vita watu wa kusini na kuteka wafungwa kama watumwa. Hivyo hadi leo uhusiano kati ya kusini na kaskazini ya nchi ni mgumu.
Tangu mwaka 2003 petroli imekuwa inaongoza kati ya bidhaa zinazopelekwa nje ya nchi badala ya pamba.
Tangu mwaka huo Mgogoro wa Darfur nchini Sudan umevuka mpaka na kuvuruga Chad pia. Ikiwa kati ya nchi zinazoongoza duniani kwa ufukara na ufisadi, ilipata shida kupokea wakimbizi kwa mamia elfu.
Ingawa kulikuwa na vyama vingi vya siasa na mapigano ya kisiasa pamoja na majaribio ya mapinduzi, mamlaka ilibaki imara mikononi mwa Rais Déby na chama chake, Patriotic Salvation Movement, hadi alipouawa mwaka 2021.
Wakazi walikuwa 15,500,000 mwaka 2018.
Jinsi ilivyo katika nchi mbalimbali za kanda la Sahel kuna aina mbili za wakazi ndani yake:
Kwa jumla leo kuna makabila zaidi ya 200 nchini, ambayo hutimia lugha na lahaja zaidi ya 100 (angalia orodha ya lugha hizo). Asili yao ni Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Afrika Magharibi na Afrika Kaskazini vilevile.
Lugha rasmi ni Kiarabu na Kifaransa.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Chad kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Chad, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.