Eire: Nchi ya visiwa katika Ulaya Kaskazini-Magharibi

Eire (pia: Ireland, Ayalandi; kwa Kiingereza mara nyingi Republic of Ireland) ni nchi ya kisiwani katika funguvisiwa la Britania ya Ulaya.

Eire

Eire ilitawaliwa na Uingereza hadi mwaka 1922. Sehemu ya kaskazini ya kisiwa imebaki kama sehemu ya Ufalme wa Muungano (pamoja na Uingereza, Uskoti na Welisi).

Mji mkuu ni Dublin.

Jiografia

Kijiografia Eire ni kisiwa kilichogawiwa kati ya Jamhuri ya Eire inayokalia sehemu kubwa ya kisiwa na Northern Ireland ambayo ni jimbo la Ufalme wa Maungano. Kisiwa chote kina eneo la km² 84,421 na 83% zake ni Jamhuri ya Eire.

Upande wa magharibi kuna Bahari ya Atlantiki, upande wa mashariki Bahari ya Eire inayokitenga na kisiwa cha Britannia.

Jiografia

Kitovu cha kisiwa kuna tambarare inayozungukwa nje upande wa pwani na vilima.

Mlima mrefu zaidi ni Carrauntoohil wenye kimo cha mita 1,038.

Mto mkubwa ni Shannon ambao kutoka kaskazini unaelekea kusini. Kwenye tambarare ya katikati kuna maziwa kadhaa.

Hali ya hewa inaathiriwa na Atlantiki: ni ya wastani, hakuna baridi kali wala joto kali.

Bahari inaleta mvua nyingi na hivyo Eire huitwa "Kisiwa cha Kijani".

Miji mikubwa ni Dublin (wakazi milioni 1), Cork (watu 190,000), Limerick (90,000), Galway (72,000) na Waterford (49,000).

Historia

Kwa karne kadhaa Eire ilitawaliwa na Uingereza.

Sheria ya mwaka 1800 iliunganisha Ufalme wa Britania Kuu na Ufalme wa Eire na hivyo kuunda Ufalme wa Muungano (United Kingdom of Great Britan and Ireland).

Baada ya Vita vya uhuru vya Eire bunge la London kwa sheria ya mwaka 1920 (Government of Ireland Act 1920) liligawa Ireland katika sehemu mbili za Northern Ireland na Southern Ireland.

Wabunge waliochaguliwa katika Ireland ya Kusini walijitangaza kuwa bunge la Eire na kwa mapatano ya mwaka 1922 uhuru wa Eire ulitambuliwa. Nchi mpya ilijiita tangu 1937 "Jamhuri ya Eire" na kuendelea kama nchi ya pekee.

Baada ya uhuru wa sehemu kubwa ya kisiwa hicho, ile ya kaskazini-mashariki imebaki kama sehemu ya Ufalme wa Muungano.

Watu

Wakazi walio wengi (82.2%) ni Waeire asili, Wazungu wengine ni 9.5%, Waasia 2.1%, Waafrika 1.2% n.k.

Wengi hutumia lugha ya Kiingereza lakini lugha ya Kieire ni lugha ya kwanza ya taifa. Kinazungumzwa katika maeneo kadhaa ya vijijini na hufundishwa shuleni, lakini kutokana na uhamiaji, Kipolandi kina wasemaji wengi zaidi.

Upande wa dini, 78.3% ni Wakatoliki na 4.2% ni Wakristo wa madhehebuya Uprotestanti na 1.3% ni Waorthodoksi. Ushiriki wa ibada ni wa juu sana. Waislamu ni 1.3% na 9.8% hawana dini.

Tazama pia

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Eire: Jiografia, Jiografia, Historia 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Serikali
    Taarifa za jumla


Nchi za Umoja wa Ulaya Eire: Jiografia, Jiografia, Historia 
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Eire: Jiografia, Jiografia, Historia  Makala hii kuhusu maeneo ya Ireland bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Eire kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Eire JiografiaEire JiografiaEire HistoriaEire WatuEire Tazama piaEire MarejeoEire Viungo vya njeEireFunguvisiwa la BritaniaKiingerezaNchi ya kisiwaniUlaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

HarmonizeVielezi vya idadiBawasiriMuundoMkoa wa DodomaAina za udongoVidonda vya tumboNdege (uanahewa)HerufiTanzaniaSayariMajina ya Yesu katika Agano JipyaTabianchiOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoDaudi (Biblia)Viungo vinavyosafisha mwiliKiraiJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaMtume BartolomayoMwenge wa UhuruYouTubeMaghaniVivumishi vya pekeeWahayaKiswahiliMkoa wa MwanzaSaa za Afrika MasharikiKiarabuJulius NyerereInjili ya MathayoLigi Kuu Tanzania BaraVivumishi vya -a unganifuMatumizi ya LughaUsafi wa mazingiraOrodha ya wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoMjombaDhahabuJiografia ya TanzaniaHoma ya manjanoMoses KulolaSamakiPemba (kisiwa)Lionel MessiMagonjwa ya kukuInjili ya YohaneWanyamweziRwandaPunyetoWapogoloAfrika Mashariki 1800-1845KonyagiVitendawiliRafikiOrodha ya kampuni za TanzaniaHistoria ya IsraelAfrika KusiniAbrahamuKitabu cha IsayaSemantikiWanyihaMbadili jinsiaMlo kamiliKichecheAfrika ya MasharikiSarufiMsalaba wa YesuMsamiatiIdi AminWallah bin WallahAbedi Amani KarumeToharaOrodha ya miji ya TanzaniaPonografiaUfahamuViwakilishi vya kuulizaMmeaUwanja wa WembleyMvua🡆 More