Sierra Leone

Sierra Leone ni nchi ya Afrika ya Magharibi.

Sierra Leone

Imepakana na Guinea na Liberia, upande wa magharibi iko bahari ya Atlantiki.

Jina la nchi lina asili ya Kireno na linamaanisha "Mlima wa Simba".

Ni koloni la zamani la Uingereza na tangu 27 Aprili 1961 ni jamhuri huru.

Sierra Leone ni kati ya nchi maskini sana duniani.

Historia

Nchi yenyewe ilianzishwa na Waingereza kwa kuunda mji wa Freetown ("Mji wa watu huru") mwaka 1787. Kusudi lake likuwa kuwarudisha Afrika watu waliowahi kuwa watumwa. Kiasili wale wakazi wa kwanza walikuwa watumwa weusi waliopewa uhuru kwa sababu walishikamana na Waingereza dhidi ya Wamarekani katika vita vya uhuru wa Marekani.

Baadaye Waingereza wapinzani wa utumwa walinunua watumwa wakiwapa uhuru na kuwapeleka Sierra Leone.

Tangu mwaka 1807 Uingereza ulikataza biashara ya watumwa (lakini utumwa wenyewe bado) na watumwa waliopatikana kwenye meli za biashara hiyo haramu walipelekwa Sierra Leone na kupewa uhuru.

Ikianzishwa na shirika la wapinzani wa utumwa Sierra Leone ikajwa koloni la kwanza la Uingereza katika Afrika ya Magharibi mwaka 1792. Kuanzia mwaka 1802 Freetown ilikuwa makao makuu ya Kiingereza kwa Afrika ya Magharibi.

Mwaka 1961 Sierra Leone ilipewa uhuru wake.

Miaka 1994 - 2002 nchi ilikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Tangu mwisho wake nchi inajengwa tena.

Watu

Wakazi asili wamegawanyika katika makabila 16, kila moja likiwa na lugha na utamaduni maalumu; kati yake makubwa zaidi ni Watemmne (35.5%) na Watembe (33.2%).

Lugha inayojulikana na asilimia 96 za wakazi ni Kikrio, aina ya Krioli ya Kiingereza iliyochanganya pia lugha mbalibali za Kiafrika. Lakini lugha rasmi ni Kiingereza.

Upande wa dini, Waislamu ni 78.5%, Wakristo ni 20.4% na wafuasi wa dini asilia za Kiafrika hawafikii 2%. Sierra Leone ni nchi isiyo na dini rasmi.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Sierra Leone 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Serikali
    Taarifa za jumla
    Vyombo vya habari
    Trade
    Tourism
    Mengineyo


Nchi za Afrika Sierra Leone 
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Sierra Leone  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sierra Leone kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Sierra Leone HistoriaSierra Leone WatuSierra Leone Tazama piaSierra Leone TanbihiSierra Leone MarejeoSierra Leone Viungo vya njeSierra LeoneAfrika ya Magharibi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Konrad LorenzMbuni (maana)TetekuwangaMkoa wa MorogoroLady Jay DeeSarafu ya BitKiburiEmmanuel MbogoMapambano ya uhuru TanganyikaOrodha ya kampuni za TanzaniaOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaPonografiaMazingiraLebanoniMzabibuUkoloniBinamuMalariaOrodha ya nchi za AfrikaWanyakyusaHarusiNuruMiikka MwambaAina ya damuHomoniFasihi simuliziMkoa wa KageraOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaLugarawaZabibuIstilahiChawaMafurikoRafikiNuktambiliMwanza (mji)Mtakatifu PauloMkoa wa MtwaraAli KibaBibliaPasakaMaadiliAustraliaPasaka ya KikristoUajemiNdege (mnyama)Doto Mashaka BitekoIsimilaHistoria ya ZanzibarLiverpool F.C.Wikipedia ya KiswahiliWafiadini wa UgandaMautiKitabu cha IsayaOrodha ya visiwa vya TanzaniaMkoa wa ArushaRicardo KakaMakabila ya IsraeliKarafuuMaumivu ya kiunoBarabaraFasihi andishiEmily Newell BlairMbwaNomino za wingiBlandina ChangulaKrioliUturukiKatumaOrodha ya vitabu vya BibliaMethaliOrodha ya Marais wa MarekaniTabianchiMbooMamaUtakatifuInjili ya YohaneMaktabaUnyenyekevu🡆 More