Serbia

Serbia (kwa Kiserbokroatia: Република Србија au Republika Srbija) ni nchi ya Ulaya kwenye rasi ya Balkani.

Serbia

Imepakana na Hungaria, Bulgaria, Romania, Masedonia Kaskazini, Kosovo (au Albania), Montenegro, Bosnia na Herzegovina na Kroatia.

Mji mkuu ni Belgrad, wenye watu milioni 1,2.

Nchi ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na inatarajia kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Historia

Waslavi walihamia Balkani baada ya karne ya 6.

Kati yao, Waserbia waliunda falme mbalimbali mwanzoni mwa Karne za Kati.

Mwaka 1217 Ufalme wa Serbia ulitambuliwa na Roma na Bizanti na mwaka 1346 ulifikia kilele cha ustawi wake kama Dola la Serbia.

Hali hiyo haikudumu muda mrefu, tena katikati ya karne ya 16 eneo lote la Serbia ya leo lilitekwa na Waosmani, ingawa pengine sehemu yake ilitawaliwa na Dola la Wahabsburg.

Mwanzoni mwa karne ya 19, mapinduzi ya Serbia ilileta ufalme wa kikatiba wa kwanza katika Balkani.

Ufalme huo ulizidi kuenea na baada ya vita vikuu vya kwanza vilivyosababisha vifo vingi vya raia zake, Serbia iliungana na makabila kuanzisha Yugoslavia iliyodumu hadi miaka ya 1990 iliposambaratika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 2006 hata Montenegro ilitengana na Serbia, ila kwa amani.

Mwaka 2008 bunge la jimbo la Kosovo lilijitangazia uhuru.

Watu

Nchi, ukiondoa Kosovo, ina wakazi 7,186,862 kwenye eneo la km² 88.361. Wengi wao wana asili ya Kislavoni.

Upande wa dini 85% ni Waorthodoksi, 5% Wakatoliki, 3% Waislamu, 1% Waprotestanti.

Serbia  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Serbia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

BalkaniKiserbokroatiaRasiUlaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

PasifikiMatumizi ya LughaKiini cha atomuUkristoMenoVivumishi vya kumilikiMartin LutherHaki za binadamuEmmanuel John NchimbiBaruaAzimio la ArushaRisalaOrodha ya wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPonografiaKiingerezaTungo sentensiFasihi andishiRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniMalawiWikipediaRose MhandoKorea KusiniKichochoMichoro ya KondoaTwigaMaskiniBibliaSaratani ya mlango wa kizaziTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaMeridianiDiplomasiaHistoria ya WapareMmeaBwehaMnyoo-matumbo MkubwaUbepariMamaWaduduBinadamuMsituNigeriaAli Hassan MwinyiMkutano wa Berlin wa 1885UkabailaMshubiriChakulaIsimuBukayo SakaMashineFani (fasihi)NathariMkoa wa MbeyaTaasisi ya Taaluma za KiswahiliNairobiSimuKukuJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaSiasaSentensiKombe la Mataifa ya AfrikaNdoaIsraeli ya KaleTasifidaTanzaniaSemiRitifaaJinaNgome ya YesuKutoka (Biblia)Mimba kuharibikaNgeliDaudi (Biblia)Uundaji wa manenoJipuOrodha ya shule nchini Tanzania🡆 More