Isaka

Isaka (kwa Kiebrania יצחק) ni jina la mwana wa Abrahamu anayetajwa katika Biblia ya Kiebrania, ambayo ni sehemu ya Biblia ya Kikristo (Agano la Kale).

Isaka
Abrahamu anazuiliwa na Mungu asimtoe Isaka kama sadaka
Uchongaji wa Andrea Mantegna kwenye altare mjini Mantua (mnamo 1461)

Habari zake zinapatikana hasa katika kitabu cha Mwanzo 21:1-22;1 n.k. na 24;1-28 n.k.

Kufuatana na habari za kitabu hicho Abrahamu alimzaa na mke wake Sara akiwa mwana wake wa pili baada ya Ismaeli aliyemwahi kuzaa na mjakazi Hagar.

Katika Biblia anatazamiwa kama mrithi halali wa Abrahamu pamoja na kupokea baraka kutokana na agano la Mungu na ukoo wa babake.

Isaka alipokuwa mtoto bado aliokolewa na malaika kwenye altare alipoelekea kuchinjwa na baba yake kama sadaka .

Alimwoa Rebeka na kuzaa naye mapacha Esau na Yakobo.

Kadiri ya Mwa 25:19-34, Rebeka alimzalia Isaka watoto pacha wenye sura na silika tofauti, Esau na Yakobo. Wa kwanza analaumiwa hasa kwa kupuuzia baraka ya Mungu iliyokuwa haki ya kifunguamimba: kwa sahani ya dengu alikubali kukosa neema zile zote alizojitwalia Yakobo kwa imani yake (Eb 12:16-17).

Mwa 27 inasimulia jinsi Yakobo, akifundishwa na mama yake, alivyoweza kubarikiwa na baba. Ingawa uongo wake haukubaliki (Hos 12:3-5), Mungu alithibitisha baraka ya Isaka kadiri ya desturi yake ya kumpendelea mdogo: hivyo Yakobo, aliyekimbia nchi yake ana fimbo tu, alirudi miaka ishirini baadaye ana wake 2, masuria 2, watoto 11 na mifugo wengi ajabu (Mwa 32). Kabla hajaingia nchi yake Mungu alishindana naye usiku kucha akalazimika kumbariki na kumtajia jina jipya, Israeli.

Isaka alipoaga dunia alizikwa na wanae kwenye pango la Makhpela karibu na mji wa Hebron.

Isaka anatajwa pia katika Kurani ya Uislamu.

Tazama pia

Viungo vya nje

Isaka  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Isaka kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

AbrahamuAgano la KaleBiblia ya KiebraniaBiblia ya KikristoKiebrania

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

LilithMadiniMapenziNdoaKifua kikuuVichekeshoAfrika ya MasharikiAlomofuRihannaMkoa wa MaraSintaksiMkoa wa MtwaraUtataWapareMwenge wa UhuruLahaja za KiswahiliFisiMatumizi ya LughaFonetikiMagonjwa ya machoMatumizi ya lugha ya KiswahiliMfumo katika sokaMkoa wa SongweOrodha ya milima ya AfrikaHali ya hewaVita ya Uingereza dhidi ya ZanzibarJumuiya ya Afrika MasharikiMamaKadi za mialikoMkoa wa TangaKiongoziKiswahiliZiwa ViktoriaJipuGridiViwakilishiKilatiniUkuaji wa binadamuUhifadhi wa fasihi simuliziARuhollah KhomeiniVirusi vya UKIMWIUzalendoKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniSanaaVipera vya semiCristiano RonaldoUfeministiViwakilishi vya sifaOrodha ya nchi kufuatana na wakaziPijiniMatendo ya MitumeMtakatifu PauloAfrika KusiniOrodha ya vitabu vya BibliaInsha ya wasifuUtandawaziKiambishi tamatiRohoJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoUenezi wa KiswahiliPijini na krioliOlduvai GorgeNomino za pekeeMbwana SamattaTabiaMaji kujaa na kupwaTenziKupatwa kwa MweziEdomuRadiChuiLugha ya kwanzaMakaburuMohammed Gulam Dewji🡆 More