Wali

Kwa Wali kama cheo tazama liwali

Wali
Wali kwa kuku kwenye sahani

Wali ni chakula kitokanacho na nafaka, hasa mbegu ya mpunga inayoitwa mchele, baada ya kazi ya kuikoboa yaani kutoa maganda yake.

Neno "wali" hutumiwa pia kwa nafaka za mtama au ngano zikipikwa, lakini kwa kawaida watu huelewa wali wa mchele.

Wali ni kati ya vyakula muhimu zaidi duniani. Kama chakula cha watu inashindana kidunia na ngano. Hasa watu wa Asia ya Mashariki na Asia ya Kusini hutegemea wali kama chakula cha kila siku.

Katika Afrika wali ni chakula cha pekee kwa watu wengi, isipokuwa pale ambako mpunga unalimwa. Nje ya hapo wali ni chakula cha sikukuu au cha nafasi ya pekee au ya matajiri.

Katika Afrika ya Mashariki chakula kinachopendwa ni kuku kwa wali au samaki kwa wali. Chakula cha pekee kabisa ni pilau ambayo ni wali unaochanganywa na viungo maalumu na nyama.

Upishi

Kuna njia mbalimbali za kupika wali. Mara nyingi hupikwa katika maji. Wapishi hupima kikombe kimoja cha mpunga na vikombe viwili vya maji na kupika hadi maji yamekwisha, hapo basi wali huwa umeiva. Wengine hupendelea kuonja mara kwa mara mpaka wameridhika. Kuna pia sufuria za umeme maalum, hasa kwa upishi wa wali.

Katika nchi kama Hispania mpunga kwanza hukaangwa katika mafuta na maji huongezwa baadaye.

Watu wengine wanapendelea kutumia supu badala ya maji kwa kuongeza utamu wa wali. Wengine hutumia pia tui la nazi.

Aina mbalimbali za mpunga huleta vyakula tofauti. Kuna wali unaotokea laini sana na aina nyingine unatokea imara zaidi.

Marejeo

Viungo vya nje

Wali  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Liwali

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KaaMoses KulolaUtandawaziShangaziMange KimambiAina za manenoShinaMatumizi ya LughaTendo la ndoaUpinde wa mvuaMkoa wa KigomaMkoa wa NjombeMeta PlatformsZana za kilimoNdoa katika UislamuWayao (Tanzania)NyangumiManchester CityChuo Kikuu cha Dar es SalaamUnyanyasaji wa kijinsiaTamthiliaSanaa za maoneshoAsili ya KiswahiliTasifidaUtumwaMazingiraBahatiMavaziUkristoOrodha ya Magavana wa TanganyikaMaana ya maishaLingua frankaStadi za maishaJangwaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoNdoto ya AmerikaMachweoWakingaShomari KapombeMuungano wa Tanganyika na ZanzibarMuundoHistoria ya KiswahiliUkimwiLigi Kuu Uingereza (EPL)Orodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaMkoa wa KageraSteven KanumbaMitume na Manabii katika UislamuFamiliaMwanaumeKabilaRufiji (mto)Mwanzo (Biblia)LongitudoKitaluMwenge wa UhuruKiwakilishi nafsiTaasisi ya Taaluma za KiswahiliBurundiWasukumaTungo kishaziAmfibiaShikamooMlongeBenjamin MkapaViwakilishiVita Kuu ya Kwanza ya DuniaKihusishiTungoTanganyika African National UnionMeliVasco da GamaTetekuwangaOrodha ya makabila ya TanzaniaMwigizaji🡆 More