Ukambi

Ukambi (au surua) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoenezwa sana kupitia mgusano yanayosababishwa na virusi vya ukambi.

Ukambi
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10B05.
ICD-9055
DiseasesDB7890
MedlinePlus001569
eMedicinederm/259 emerg/389 ped/1388
MeSHD008457

Ishara na dalili za kwanza kwa kawaida hujumuisha homa, ambayo mara nyingi huwa zaidi ya °C 40 (°F 104.0), kikohozi, mafua, na macho mekundu. Siku mbili au tatu baada ya dalili kuanza, madoa madogo meupe yanaweza kuonekana ndani ya kinywa yanayojulikana kama alama za koplik. Chunusi nyekundu, zinazoanza kwenye uso kisha kuenea kwa mwili wote, kwa kawaida huanza siku tatu hadi tano baada ya mwanzo wa dalili.

Dalili kwa kawaida huwa siku 10–12 baada ya kutangamana na mtu aliyeambukizwa kwa siku 7–10.

Matatizo zaidi ya ukambi hutokea kwa takriban asilimia 30 na yanaweza kujumuisha kuhara, upofu, inflamesheni ya ubongo, na nimonia miongoni mwa mengine.

Rubela na roseola ni magonjwa tofauti ingawa yanafanana na surua.

Kisababishi na utambuzi

Ukambi ni ugonjwa unaoambukiza kupitia hewa na kuenezwa kwa urahisi na watu walioambukizwa kupitia kikohozi na kupiga chafya. Pia unaweza kuenezwa kupitia kutangamana na mate au makamasi. Watu tisa kati ya kumi wasio na kingamwili wanaokaa pamoja na mtu aliyeambukizwa wataambukizwa ukambi. Watu huweza kuwaambukiza wengine katika siku nne kabla hadi siku nne baada ya mwanzo wa chunusi.

Watu kwa kawaida hupata ugonjwa huu mara moja tu. Vipimo vya virusi hivi katika visa vinavyokisiwa ni muhimu kama sehemu ya juhudi za afya ya umma.

Kinga na tiba

Chanjo ya ukambi huwa mwafaka katika kuzuia ugonjwa huu. Uchanjaji umepunguza asilimia 75 ya vifo vilivyotokana na ukambi kati ya miaka ya 2000 na 2013 na takriban asilimia 85 ya watoto ulimwenguni kote wanapata chanjo kwa sasa.

Hakuna matibabu maalum ya ukambi. Hata hivyo, utunzaji wa kimsaada unaweza kuboresha matokeo. Hii inaweza kujumuisha kuwapa wagonjwa mmumunyo wa chumvi-maji za kunywa (viowevu vyenye utamu na chumvi), vyakula vyenye afya na dawa ya kupunguza homa. Antibiotiki zinaweza kutumika ikiwa maambukizi ya bakteria kama vile ya numonia yatatokea. Nyongeza ya Vitamini A hupendekezwa katika nchi zinazoendelea.

Epidemiolojia na prognosisi

Ukambi huathiri takriban watu milioni 20 kila mwaka, hasa katika maeneo yanayoendelea barani Afrika na Asia. Ukambi husababisha vifo vingi vinavyoweza kuzuiwa kwa kutumia chanjo ikilinganishwa na magonjwa mengine. Ukambi ulisababisha takriban vifo 96,000 katika mwaka wa 2013 ikilinganishwa na vifo 545,000 katika mwaka wa 1990. Katika mwaka wa 1980, ugonjwa huu ulikadiriwa kusababisha vifo milioni 2.6 kila mwaka. Kabla ya uchanjaji nchini Marekani, kati ya visa milioni tatu na milioni nne vilitokea kila mwaka. Watu wengi wanaoambukizwa na kufariki huwa wenye umri wa chini ya miaka mitano. Hatari ya kifo kwa walioambukizwa kwa kawaida huwa asilimia 0.2, lakini hii inaweza kuongezeka hadi asilimia 10 kwa wale walio na utapiamlo. Ukambi hauaminiki kuathiri wanyama.

Marejeleo

Tags:

Ukambi Kisababishi na utambuziUkambi Kinga na tibaUkambi Epidemiolojia na prognosisiUkambi MarejeleoUkambiUgonjwa wa kuambukiza

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Ndoto ya AmerikaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoMwigizajiMfumo wa upumuajiUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaKipepeoSaida KaroliSaidi NtibazonkizaUgonjwaTaasisi ya Taaluma za KiswahiliAlfabetiMnyoo-matumbo MkubwaMkoa wa MbeyaMziziJiografia ya TanzaniaMichezoMweziTanganyika African National UnionMoses KulolaUti wa mgongoNguzo tano za UislamuInsha ya wasifuMajiDNAMkoa wa Dar es SalaamNyotaWazaramoMadiniMbuga za Taifa la TanzaniaBarack ObamaNuktambiliHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoMashineKukuIrene UwoyaCherehaniVivumishi vya urejeshiKata za Mkoa wa Dar es SalaamMapambano kati ya Israeli na PalestinaHadithi za Mtume MuhammadKisononoIsraelBarua pepeMavaziMkoa wa NjombeKiunzi cha mifupaAlama ya uakifishajiKitaluMisemoMkoa wa MaraKidoleOrodha ya Magavana wa TanganyikaMahakamaLuka ModricShinikizo la juu la damuNileMnyamaWahangazaZuchuSteve MweusiLilithMfumo wa JuaNomino za wingiKamusi elezoWawanjiAmri KumiMlongeOrodha ya majimbo ya MarekaniKanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli🡆 More