Ufini: Nchi katika Ulaya Kaskazini

Ufini (kwa Kifini: Suomi) ni nchi ya Skandinavia iliyoko Ulaya ya Kaskazini.

Imepakana na Norwei upande wa kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi. Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia ambayo watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani, lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.

Ufini
Ufini: Historia, Watu, Watu maarufu
Pielinen

Nchi ina wakazi milioni tano unusu tu katika eneo la km² 338,000; hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano mdogo wa watu. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu. Mji mkuu ni Helsinki; mji muhimu mwingine ni Tampere, mji ulioko karibu kilomita 180 kaskazini mwa Helsinki, ni wa pili kwa ukubwa. Miji mingine mikubwa ni pamoja na Turku, Kuopio na Vaasa.

Ufini ilijitegemea mnamo 1917. Kati ya 1939 na 1944, Ufini ilipigana dhidi ya Umoja wa Kisovyeti na jeshi la Ufini liliongozwa na kamanda Carl Gustaf Emil Mannerheim.

Nchi ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya.

Historia

Historia ya awali

Ufini ulikaliwa na watu tangu ilipokwisha enzi ya barafu ya mwisho, miaka 9000 KK hivi. Wakazi wa kwanza walikuwa wawindaji-wakusanyaji ambao walitumia vifaa vya mawe vinavyofanana na vile vya Estonia, Russia na Norway.

Labda kilimo kilianza miaka 3000 KK - 2500 KK.

Karne za kati

Mwishoni mwa karne ya 13 Ufini ukawa sehemu ya Sweden hadi mwaka 1809, ilipomezwa na Urusi kama ufalme mdogo wenye kujitawala kwa kiasi fulani.

Karne ya 20

Ufini: Historia, Watu, Watu maarufu 
Carl Gustaf Emil Mannerheim

Mwaka 1906, Ufini ulikuwa nchi ya kwanza duniani kuwapa wananchi wote wenye umri wa utu uzima haki ya kugombea vyeo vya serikali.

Mwaka 1917, baada ya Mapinduzi ya Russia, Ufini ulijitangaza huru na mwaka uliofuata ukawa jamhuri baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wakati wa vita vikuu vya pili, Muungano wa Kisovyeti ulijitahidi kuteka Ufini wote, ukaishia kutwaa Karelia, Salla, Kuusamo, Petsamo na visiwa kadhaa tu.

Baada ya vita Ufini uliacha kutegemea kilimo ukajitosa katika uchumi wa viwanda hata kufikia kuwa kati ya nchi zilizoendelea zaidi.

Mwaka 1955 Ufini ulijiunga na Umoja wa Mataifa ukichagua siasa ya kutoambatana na upande wowote.

Mwaka 1995 ulijiunga na Umoja wa Ulaya na mwaka 1999 ulikubali kutumia euro.

Watu

Ufini: Historia, Watu, Watu maarufu 
Ufini inajulikana kama "Nchi ya Maziwa Maelfu".

Kuna jumuiya tatu katika Ufini:

  • Wafini wenyewe ambao ni 90% ya wakazi wote.
  • Waswidi wako hasa upande wa kusini mwa nchi, kwa jumla ni takriban 5% ya wakazi; hasa visiwa vya Aland kuna Waswidi watupu walio na hali ya kujitawala ndani ya Ufini.
  • Wakazi asilia ni Wasami ambao wako kaskazini tu. Maisha yao yanategemea uwindaji na ufugaji; wako wachache, jumla yao haifikii 0.2% ya wakazi wote.

Mbali na hao, kuna wahamiaji (5.9%), hasa kutoka Russia, Estonia na Somalia.

Lugha rasmi ni Kifini na Kiswidi. Lugha ya Kifini ina asili ya Asia ya Kati, haina uhusiano na lugha za Kihindi-Kiulaya.

Wakazi wenye lugha ya Kiswidi wako upande wa kusini mwa nchi kwa sababu Ufini ilitawaliwa na Uswidi kwa karne nyingi. Katika karne hizo walikuwepo Waswidi waliohamia Ufini lakini kuna pia Wafini walioanza kutumia Kiswidi pekee. Hasa kwenye visiwa vya Aland Kiswidi ni lugha pekee. Lakini Waswidi wa Ufini wanajisikia wa Ufini.

Upande wa dini, 72% ni Walutheri na 1.1% Waorthodoksi. Madhehebu hayo mawili ya Ukristo yanatambulika na kupewa nafasi katika matukio mbalimbali na shuleni. 1,6% wanafuata dini au madhehebu mengine, wakati 25.3% hawana dini yoyote.

Watu maarufu

  • Mikael Agricola
  • Urho Kaleva Kekkonen
  • Elias Lönrrot
  • Garlf Gustaf Emil Mannerheim
  • Martti Ahtisaari
  • Alvar Aalto
  • Jean Sibelius

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Ufini: Historia, Watu, Watu maarufu 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:


Nchi za Umoja wa Ulaya Ufini: Historia, Watu, Watu maarufu 
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Ufini: Historia, Watu, Watu maarufu  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Ufini HistoriaUfini WatuUfini Watu maarufuUfini Tazama piaUfini TanbihiUfini Viungo vya njeUfiniBaltikiEstoniaKaskaziniKifiniLughaMagharibiMasharikiMawasilianoNorwaySkandinaviaUlaya ya KaskaziniUrusiUswidi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

NimoniaNgano (hadithi)Nomino za jumlaSensaVihisishiAla ya muzikiKitenziStephane Aziz KiSerie AZodiakiDiniLingua frankaKisaweMitume na Manabii katika UislamuWazaramoHuzuniLugha rasmiMishipa ya damuApril JacksonUtamaduniKipazasautiDesturiJinsiaTafsiriOrodha ya makabila ya TanzaniaAfrika Mashariki 1800-1845SayansiUislamuMamba (mnyama)Che GuevaraKongoshoRiwayaJinaSheriaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaKumaNahauTashbihaUtohoziMaradhi ya zinaaBomu la nyukliaSarufiTiktokKitenzi kikuu kisaidiziNigeriaUharibifu wa mazingiraTahajiaSteven KanumbaYvonne Chaka ChakaKilatiniInshaHuduma ya ujumbe mfupiTanzaniaCristiano RonaldoDayolojiaJokofuNduniMsitu wa AmazonVichekeshoMtakatifu PauloMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaEe Mungu Nguvu YetuAzimio la ArushaRoho MtakatifuKunguniWachaggaHifadhi ya NgorongoroMalebaMatumizi ya LughaMtaalaUenezi wa KiswahiliOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaDodoma (mji)Mfumo katika soka🡆 More