Somalia

Somalia (kwa Kisomali: Soomaaliya), ambayo inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia, ni nchi kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki katika Pembe ya Afrika.

Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia (Kiswahili)
Jamhuuriyadda Federaalka Soomaaliya (Kisomali)
Bendera ya Somalia Nembo ya Somalia
(Bendera ya Somalia) (Nembo ya Somalia)
Lugha rasmi Kisomali
Mji Mkuu Mogadishu
Mji Mkubwa Mogadishu
Serikali Shirikisho la Jamhuri
Rais Mohamed Abdullahi Mohamed
Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble
Eneo km² 637,657
Idadi ya wakazi 17,066,000 (2022)
Wakazi kwa km² 27.2
Uchumi nominal Bilioni $7.9
Uchumi kwa kipimo cha umma $716
Pesa Shilingi ya Somalia
Kaulimbiu "Soomaaliyeey toosoo"(Wasomali waamke)
Wimbo wa Taifa Qolobaa Calankeed (Tuabudu bendera)
Somalia katika Afrika
Saa za Eneo UTC +3 (Wakati wa Afrika Mashariki)
Mtandao .so
Kodi ya Simu +252

Somalia
Ramani ya mikoa ya Somalia.

Kijiografia, imezungukwa upande wa kaskazini-mashariki na Ethiopia na Jibuti, na upande wa magharibi ya kati na Kenya; Ghuba ya Aden nayo iko mashariki.

Mji mkuu na mji mkubwa zaidi ni Mogadishu (wakazi 2,120,000).

Jiografia

    Makala kuu: Jiografia ya Somalia

Historia

Somalia 
Mji wa Bosaso, Somalia.

Ukoloni wa Italia

Kuanzia mwaka 1888 Italia ilijipatia mikataba ya ulinzi na masultani mbalimbali waliotawala maeneo madogo kwenye Pembe ya Afrika. Walitangulia 1889 na sultani ya bandari ya Hobyo na mtawala wa usultani wa Majerteen.

Mwaka 1892 Usultani wa Zanzibar ulikodisha bandari ya Banadir kati ya Mogadishu hadi Brava kwa Italia. Mwaka 1905 Italia ilinunua eneo hili kutoka Zanzibar na kulitangaza kuwa koloni na Mogadishu kuwa mji mkuu.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waitalia walikabidhiwa na Uingereza eneo la Kismayu. Walilitawala kwa jina la "Oltre Giuba" (ng'ambo ya mto Juba) na kuliunganisha na Somalia ya Kiitalia tarehe 30 Juni 1926.

Wakati uleule waliamua kumaliza hali ya sultani za Majarteen na Hobyo kuwa nchi lindwa na kuzifanya sehemu kamili za koloni. Mipango hiyo ilisababisha vita kali ya miaka miwili kwa sababu masultani waliona mikataba yao ya ulinzi ilivunjwa wakapinga jeshi la Italia.

Mwaka 1936 Somalia ikaunganishwa na Ethiopia kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kiitalia.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia makoloni ya Italia yalivamiwa na Uingereza uliotawala Somalia tangu 1941.

Mwaka 1949 Somalia ilirudishwa mikononi mwa Italia ilisimamie kwa niaba ya Umoja wa Mataifa.

Ukoloni wa Uingereza

Uingereza uliingia katika eneo hili baada ya Misri kuondoka mwaka 1885 kwa kushindwa na jeshi la Mahdi huko Sudan. Uingereza uliingia kwa sababu iliona umuhimu wa kutawala pande zote mbili za Bab el Mandeb ikihofia uenezaji wa nchi nyingine za Ulaya, hasa Ufaransa iliyokuwa na koloni la kwanza ya Ubuk (Obok) katika Jibuti ya leo tangu 1862. Pamoja na hayo Waingereza walitegemea kununua nyama kwa ajili ya mji wa Aden na meli zilizopita hapo kati ya Uhindi na Ulaya.

Somaliland ilitawaliwa awali kama mkoa wa Uhindi wa Kiingereza ikawa baadaye chini ya wizara ya makoloni huko London.

Somalia 

Hata kama Uingereza haukuwa na nia ya kuingilia mno maisha ya wenyeji ulikutana na upinzani mkali kuanzia mwaka 1899 kutoka kwa kiongozi wa dini Diiriye Guure, aliyeitwa na Waingereza "Mullah majununi". Waingereza walijibu kwa ukatili katika vita vya miaka 20 iliyoua takriban theluthi moja ya wakazi wote wa eneo.

Mwishowe Uingereza iliweza kumaliza upinzani kwa teknolojia mpya ya eropleni za kijeshi zilizotumia mabomu na bunduki za mtombo kutoka angani kwa mara ya kwanza katika Afrika.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia eneo likatwaliwa na Italia katika Agosti 1940 lakini lilichukuliwa tena na Uingereza katika Machi 1941.

Uhuru

Mwaka 1960 utawala wa kikoloni ulikwisha na Somalia ikapata uhuru wake, ikiunganisha makoloni mawiliː la Waitalia (kusini) na la Waingereza (kaskazini).

Baada ya mwaka 1991 nchi ya Somalia ilibaki haina serikali wala umoja wa taifa, bali iligawiwa na wakereketwa na wanamgambo wa ukoo na eneo, hasa Somaliland, Puntland na Galmudug upande wa kaskazini.

Katika miaka 2008-2013 ilihesabika kama nchi filisika. Kwa sasa ni nchi dhaifu lakini inaanza kujengwa upya kama shirikisho na kujiandaa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tarehe 4 Machi 2024 imejiunga rasmi na Jumuia ya Afrika Mashariki.

Somalia 
Klipspringers anaishi katika maeneo ya milimani yenye mimea kidogo.

Watu

Tazama pia: Orodha ya lugha za Somalia

Somalia 
Hii ramani ya mwaka 2002 inaonyesha msongamano wa watu nchini.

Wakazi asili wa Somalia ni Wasomali (85%) wa makabila yafuatayo:

    • Isaaq
    • Hawiye
    • Dir
    • Darod
    • Digil & Mifle

Wengine (15%) ni:

Somalia 
Ramani ikionyesha uenezi wa lugha ya Kisomali katika Pembe la Afrika.

Kisomali ndiyo lugha ya kawaida ya wakazi wengi na lugha rasmi pamoja na Kiarabu. Kati ya lugha nyingine zinazotumika nchini, mojawapo ni Kiswahili (lahaja za Chimbalanzi na Kibajuni).

Upande wa dini, 99.8% ni Waislamu, hasa Wasuni. Wakristo hawafikii 0.1%.

Somalia 
Somali lahoh (canjeero).
Somalia 
Maporomoko ya maji ya Lamadaya kwenye mlima Cal Madow.
Somalia 
Eneo la Somaliland.
Somalia 
Mandhari ya milima ya Cal Madow, makao ya spishi nyingi za pekee.
Somalia 
Ufukwe wa Berbera.
Somalia 
Dahabshiil huko Hargeisa.
Somalia 
Duka huko Burao.
Somalia 
Hargeisa International Airport huko Hargeisa.
Somalia 
Watu mjini Hargeisa.

Utawala

Maeneo (umoja: gobolka, wingi: gobollada) ya Somalia, ambayo imegawiwa tena katika wilaya, ni 18:

Mikoa ya Somalia
Mkoa Eneo (km2) Wakazi Makao makuu
Awdal 21,374 1,010,566 Borama
Bari 70,088 719,512 Bosaso
Nugal 26,180 392,697 Garowe
Mudug 72,933 717,863 Galkayo
Galguduud 46,126 569,434 Dusmareb
Hiran 31,510 520,685 Beledweyne
Shebeli wa Kati 22,663 516,036 Jowhar
Banaadir 370 1,650,227 Mogadishu
Shebeli wa Chini 25,285 1,202,219 Barawa
Togdheer 38,663 721,363 Burao
Bakool 26,962 367,226 Xuddur
Woqooyi Galbeed 28,836 1,242,003 Hargeisa
Bay 35,156 792,182 Baidoa
Gedo 60,389 508,405 Garbahaarreey
Juba wa Kati 9,836 362,921 Bu'aale
Juba wa Chini 42,876 489,307 Kismayo
Sanaag 53,374 544,123 Erigavo
Sool 25,036 327,428 Las Anod
Somalia 
Banda la biashara huko Mogadishu.

Mawasiliano

Mawasiliano ya Jamhuri ya Somalia ilikaribia kuangamia kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini kwa sasa kampuni za binafsi za mawasiliano ya mitambo, zimetwaa karibu miji yote Somalia, na hata kutoa huduma njema kuliko nchi zilizo jirani.

Somalia ni nchi mojawapo Afrika ambayo ina mawasiliano ya bei rahisi zaidi, pengine kwa kuwa Somalia haikuwa na serikali iliyotoza ushuru; (Telecoms thriving in lawless Somalia) Kampuni zinazohudumia watu wa Somalia ni kama:

  • SOMTEL
  • Galkom
  • Global Internet Company
  • Hormuud
  • Telcom
  • Nationlink
  • Netco
  • STG
  • Dahabshiil

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  •  
  •  
  •  
  •  
  •  
  • Mauri, Arnaldo, Somalia, in G, Dell'Amore (ed.), "Banking Systems of Africa", Cariplo-Finafrica, Milan, 1971, pp. 209–217.[1]
  •  
  • In Lowell W. Barrington, ed., After Independence: Making and Protecting the Nation in Postcolonial and Postcommunist States (pp. 107–137). Ann Arbor, MI: University of Michigan Press. ISBN 978-0-472-09898-9. 
  • Shay, Shaul. Somalia in Transition Since 2006. Piscataway, NJ: Transaction Publishers, 2014.
  •  
  •  

Viungo vya nje

Somalia 
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Habari, mitandao inayojadili kuhusu Somalia.
    Habari za kawaida
    Watambuzi


Nchi za Afrika Somalia 
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Somalia  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Somalia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Somalia JiografiaSomalia HistoriaSomalia WatuSomalia UtawalaSomalia MawasilianoSomalia Tazama piaSomalia TanbihiSomalia MarejeoSomalia Viungo vya njeSomaliaAfrika ya MasharikiKisomaliPembe ya AfrikaPwani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Azimio la ArushaChuiVita Kuu ya Pili ya DuniaUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaAlbert EinsteinBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiMorokoHistoria ya WapareNdotoUtoaji mimbaUfahamuUgonjwa wa kuharaLugha ya kwanzaMaadiliOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaTaswira katika fasihiUtawala wa Kijiji - TanzaniaBahari ya HindiOrodha ya kampuni za TanzaniaOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaKimondo cha MboziMadawa ya kulevyaRaiaJackie ChanKitufeVita ya Maji MajiChristina ShushoUsimbajiWasukumaWahayaKichochoMkoa wa ArushaUtapiamloKitenziOrodha ya vitabu vya BibliaOrodha ya makabila ya TanzaniaMbeguMwakaOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaUkuaji wa binadamuJamhuri ya Watu wa ChinaOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaBawasiriKamusi za KiswahiliEnglish-Swahili Dictionary (TUKI)AmfetaminiZodiakiHifadhi ya NgorongoroHali ya hewaMaadili ya kiutuAngahewaJuxFIFABikiraNdoa katika UislamuArsenal FCAlhamisi kuuMkoa wa MwanzaUturukiMkoa wa ManyaraRihannaNembo ya TanzaniaMandhariMofolojiaMuda sanifu wa duniaUdongoMoyoAlama ya barabaraniVivumishi vya -a unganifuHistoria ya AfrikaWachaggaKaswende🡆 More