Jamhuri ya Madagaska (au Madagasikari) inaenea katika kisiwa cha Madagaska (pia: Bukini) kilichopo katika Bahari Hindi mashariki kwa pwani ya Afrika.
| |||||
Wimbo wa Taifa: Tanindrazana, Fahafahana, Fandrosoana (kwa Kimalagasi: Nchi ya wenyeji, Uhuru, Maendeleo) | | |||||
Lugha rasmi | Kimalagasi Kifaransa | ||||
Mji Mkuu | Antananarivo | ||||
Rais Waziri Mkuu | Andry Rajoelina Christian Ntsay | ||||
Eneo - Jumla - 0.9% Maji | Ya 46 duniani km² 587,041 | ||||
Umma - Kadirio (Ya 52 duniani) - Jumla (26,262,313 ) - Umma kugawa na Eneo 35.2 | Ya 174 duniani ; (Ya 142 duniani) | ||||
GDP Chumo cha uchumi - Jumla - kwa kipimo cha umma | 126 kadir $15.82 billion (223) $900 (214) | ||||
Uhuru | 26 Juni 1960 | ||||
Fedha | Ariari | ||||
Saa za Eneo | UTC +3 | ||||
Wimbo wa Taifa | Ry Tanindraza nay malala ô (Eh, nchi yetu asili) | | ||||
Intaneti TLD | .mg | ||||
kodi za simu | 261 | ||||
1Lugha ya Malagasi, kulingana na katiba ndiyo lugha ya Taifa. Lugha ya Kifaransa, haijatiwa umaakini kama Lugha rasmi. |
Jina Madagaska lina maana ya "Kisiwa kikubwa" na linatokana na lugha ya wenyeji, Wamalagasi ambao waongea Kimalagasi.
Kisiwa chenyewe ni cha nne kwa ukubwa duniani.
Upekee wa kisiwa unatokana na kwamba kilimeguka kutoka India miaka milioni 88 hivi iliyopita, halafu kilibaki bila watu hadi karne ya 5 hivi BK.
Kisiwa hicho ni pia mazingira makubwa ya aina ya violezo ambayo ni asilimia 5 ya violezo vyote vya mimea na wanyama vya dunia nzima.
Asilimia 90 ya viumbehai asili ni maalumu wa Madagaska, kama vile wanyama aina ya kima awali wanaoitwa lemuri, ndege ambao waambukiza ugonjwa na mti wa mbuyu.
Madagaska ni kati ya maeneo ya mwisho kufikiwa na kukaliwa na binadamu.
Wa kwanza kufika walitokea visiwa vya Indonesia (kama mwaka 350-550 BK).
Baadaye tu walihamia watu kutoka bara la Afrika (mwaka 1000 hivi) na wengineo (Waarabu, Wahindi, Wazungu, Wachina n.k.).
Kuanzia mwaka 1787 hadi mwaka 1897 kisiwa kilizidi kuunganishwa kisiasa chini ya Ufalme wa Merina.
Watawala walikuwa watu kutoka familia ya Andrianampoinimerina, mwanzilishi wa taifa hilo, ambaye alikuwa ametokea katika kabila la Wamerina
Kabila hilo lilikuwa kubwa na muhimu kuliko yote 18 ya kisiwa hicho. Makazi yake yalikuwa katika uwanda wa juu wa kati lakini lilienea sehemu kubwa ya Bukini.
Wamerina walikuwa na makao makuu ya utawala wao Antananarivo; baada ya kugawiwa kwa ufalme wao mnamo 1710 kitovu cha malaka kati ya Wamerina ikahamia kwenye mlima wa Ambohimanga lakini tangu kuunganishwa kwa Wamerina mnamo 1794 mji mkuu ukulikuwa tena Atananarivo. Kutoka hapo waliweza kueneza mamlaka yao katika sehemu nyingine za kisiwa hicho.
Makabila yote ya wenyeji yalizungumza lugha moja na yalikuwa na mila na desturi zinazofanana, hivyo yaliweza kujenga umoja wa kiutamaduni uliowafanya wawe jamii moja kimsingi.
Watawala hao wa kifalme waliweza kutekeleza mambo mbalimbali kuendeleza Bukini katika vipindi vyao kabla ya kuja kwa wageni kutoka Uingereza na Ufaransa ambao kwa kiasi fulani ulidhoofisha mamlaka ya kifalme.
Kisiwa hicho hatimaye kiligeuzwa kuwa koloni la Ufaransa. Hii ni kwa kuwa, ingawa sera ya kuisasisha ya Bukini kwa namna fulani iliimarisha uwezo wa nchi hiyo wa kutetea uhuru wake, lakini kwa ujumla sera hiyo ilidhoofisha ufalme huo kwa kuongeza utegemezi wake kwa mataifa ya kigeni.
Mwaka 2018 idadi ya wakazi ilikadiriwa kuwa milioni 26.3. Wenyeji wengi wana mchanganyiko wa damu: DNA inaonyesha kuwa wakazi wa kwanza kutoka Indonesia wameichangia asilimia 50 hivi na Waafrika vilevile. Wanaoishi sehemu za ndani ni wa Kiindonesia zaidi, wakati wale wa pwani ni wa Kiafrika zaidi.
Lugha ya taifa ni Kimalagasi. Lugha rasmi za Madagaska ni Kimalagasi na Kifaransa (angalia pia orodha ya lugha za Madagaska).
Mwaka 1993 nchini Madagaska kulikuwa na dini za jadi (52% hivi), Ukristo (41%, Waprotestanti wakiwazidi kidogo Wakatoliki), Uislamu (7% hivi) n.k. Tangu hapo wafuasi wengi wa dini za jadi wameongokea Ukristo, hasa wa Kiprotestanti.
Pamoja na kutokea mazingira tofauti sana, Wamalagasi wamechanganyikana sana na kuwa na utamaduni na lugha aina moja, ya Kiindonesia zaidi.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Madagaska kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Madagaska, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.