Kifafa

Kifafa (kwa Kiingereza Epilepsyis, kutoka kitenzi cha Kigiriki ἐεπιλαμβάνειν, eepilambanein, kuteka au kutesa) ni kundi la maradhi ya neva yanayofanana kwa dalili za matukio ya kupatwa, ambayo yanaweza kudumu muda mfupi sana karibu bila kugundulika hadi muda mrefu wa kutikisika kwa nguvu mwili mzima.

Matukio hayo yanaelekea kurudiarudia bila sababu inayoeleweka kwa kila tukio wakati matukio ya namna hiyo yenye sababu inayoeleweka si ya kifafa kweli.

Picha za video kuhusu matukio ya kifafa.
Kifafa
Majeraha ulimini yaliyosababishwa na anguko.

Visababishi

Sababu ya kesi nyingi haijulikani, ingawa baadhi ya watu wanapatwa na kifafa kutokana na jeraha la ubongo, kiharusi, saratani ya ubongo na matumizi mabaya ya dawa. Mabadiliko ya DNA yanahusiana moja kwa moja na asilimia ndogo za kesi zote.

Matukio ya kifafa yanatokana na utendaji mkubwa mno wa neva za ubongo.

Ili kusema ni kifafa, daktari anapaswa kwanza kutambua hakuna sababu zinazoeleweka za dalili kama hizo, kwa mfano kuzimia. Mara nyingi kifafa kinaweza kuthibitishwa na electroencephalogram (EEG).

Tiba

Katika 70% za matukio inawezekana kuyadhibiti. Isipowezekana tiba, pengine upasuaji, uchocheaji wa neva na mabadiliko ya ulaji vinatumika. Si kila mara kifafa kinadumu maisha yote: kuna watu wanaopata nafuu kiasi cha kutohitaji tena dawa.

Uenezi

Karibu 1% ya watu wote duniani (milioni 65) wana kifafa, na karibu 80% za kesi zinatokea katika nchi zinazoendelea.

Mwaka 2013 vilitokea vifo 116,000, ambavyo ni vingi kuliko vile 112,000 vya mwaka 1990.

Kifafa kinazidi kutokea kadiri watu wanavyokua.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • World Health Organization, Department of Mental Health and Substance Abuse, Programme for Neurological Diseases and Neuroscience; Global Campaign against Epilepsy; International League against Epilepsy (2005). Atlas, epilepsy care in the world, 2005 (pdf). Geneva: Programme for Neurological Diseases and Neuroscience, Department of Mental Health and Substance Abuse, World Health Organization. ISBN 92-4-156303-6. 

Viungo vya nje

Kifafa 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Kifafa  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kifafa kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Kifafa VisababishiKifafa TibaKifafa UeneziKifafa Tazama piaKifafa TanbihiKifafa MarejeoKifafa Viungo vya njeKifafaDaliliKigirikiKiingerezaKitenziKundiMudaMwili

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Lugha fasahaMaajabu ya duniaMamba (mnyama)TetekuwangaAdhuhuriUzazi wa mpangoAdolf HitlerShinikizo la juu la damuUrusiFalsafaDini asilia za KiafrikaKilatiniWilaya ya UkereweMsokoto wa watoto wachangaWasukumaUfahamuTiktokKaswendeTarakilishiMkoa wa KigomaMzabibuShengNguruwe-kayaLigi ya Mabingwa AfrikaMilaMagonjwa ya machoMajigamboKiimboUharibifu wa mazingiraKanisaKiraiEdomuNdoa katika UislamuMafarisayoUajemiMji mkuuVasco da GamaMlongeShahawaMaigizoNahauElimuMkoa wa KageraLigi ya Mabingwa UlayaVivumishi vya sifaTabiaUmoja wa MataifaEdward SokoineSaratani ya mlango wa kizaziMpwaNyotaWema SepetuLahajaMkoa wa RuvumaJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaTungo kiraiIbadaUbatizoKatibaTabianchi ya TanzaniaOrodha ya viwanja vya michezo TanzaniaMichezo ya watotoWabondeiChakulaKalenda ya KiislamuUenezi wa KiswahiliKaaNazi (tunda)FisiMauaji ya kimbari ya RwandaVieleziViwakilishi vya kumilikiHifadhi ya SerengetiVita vya KageraPunyetoOmbwe🡆 More