Jiolojia

Jiolojia (kutoka Kigiriki γῆ ge „ardhi“ na λόγος logos, somo, mafundisho“ = geologia - kwa matamshi ya Kiingereza jiolojia) ni fani ya sayansi inayochunguza maumbile ya dunia na tabia zake za kifizikia na kikemia.

Inachungulia pia historia ya dunia na nguvu zinazoendelea kubadilisha maumbile ya dunia.

Jiolojia
Wanajiolojia wakichunguza sampuli za mwamba zilizopatikana kwa njia ya kekee.

Neno "geologia" liliwahi kutumiwa mara ya kwanza mnamo 1778 na Mfaransa Jean-André Deluc (17271817).

Jiolojia inatazama mawe na ardhi ikitafuta maelezo kwa umbo na tabia zake kuligana na kanuni za kisayansi.

Kuna masomo madogo ndani ya jiolojia kama vile:

  • Petrolojia ni elimu ya mawe na miamba
  • Mineralojia ni elimu ya madini
  • Jiolojia ya kihistoria ni elimu ya matokeo yaliyosababisha kutokea kwa mawe, miamba, milima na mabara jinsi yalivyo leo
  • Paleontolojia ni elimu ya visukuku (mabaki ya miili ya wanyama wa kale yaliyokuwa kama mwamba)
  • Hidrojiolojia ni elimu ya hali ya maji chini ya uso wa dunia
  • Volkenolojia ni elimu ya volkeno kwenye mabara au chini ya bahari

Aina za miamba

Jiolojia inachunguza hasa miamba na kutofautisha aina tatu kufuatana na misingi yake:

  • Mwamba Moto: mwamba wa mgando au mwamba wa kivolkeno unajitokeza pale ambako magma au zaha (lava) inaganda.
  • Mwamba Tabaka: mwamba mashapo hutokea pale ambako miamba inavunjika na kusagwa katika mmomonyoko na mashapo yanakandamizwa kwa njia ya kanieneo ya mashapo ya juu hadi mashapo kuwa mwamba mapya.
  • Mwamba Geu: mwamba metamofia ni mageuzi ya miamba ya awali -ama ya kivolkeno au ya mishapo- kwa njia ya kanieneo kubwa sana na joto kali kuwa aina mpya ya mwamba. Metamofosi kwa kawaida hutokea katika kina kubwa.

Ardhi

Asili ya ardhi ni miamba iliyovunjikavunjika na kuchanganyika na mabaki ya mimea na wanyama waliooza.

Picha

Viungo vya nje

Jiolojia 
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

Jiolojia Aina za miambaJiolojia ArdhiJiolojia PichaJiolojia Viungo vya njeJiolojiaDuniaFaniFizikiaKemiaKigirikiKiingerezaMatamshiMaumbileSayansiTabia

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Bob MarleyMalengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifaKisaweMandhariAmfibiaHifadhi ya SerengetiLongitudoInshaHerufi za KiarabuUandishi wa barua ya simuZama za ChumaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaNomino za pekeeMbuniUgonjwa wa kuharaMkoa wa NjombeYvonne Chaka ChakaMaliasiliNdege (mnyama)Fani (fasihi)KukuAzimio la Kimataifa juu ya Haki za BinadamuKiongoziMazingiraKata (maana)Ligi Kuu Uingereza (EPL)Vivumishi ya kuulizaMbooWilliam RutoMajira ya mvuaMkoa wa MorogoroMkoa wa MbeyaOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaUlayaUjerumaniKonsonantiOrodha ya Marais wa BurundiLatitudoMoses KulolaVipera vya semiMkoa wa SongweOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoUzazi wa mpango kwa njia asiliaBomu la nyukliaBilioniMauaji ya kimbari ya RwandaJogooKishazi tegemeziKumamoto, KumamotoWayahudiSamakiBibliaMaudhui katika kazi ya kifasihiTupac ShakurBaraHuduma ya ujumbe mfupiChe GuevaraOrodha ya vitabu vya BibliaBiblia ya KikristoMaambukizi ya njia za mkojoMpira wa miguuLugha ya taifaDamuMbuyuPijini na krioliNandyUenezi wa KiswahiliMkoa wa SimiyuUundaji wa manenoLigi ya Mabingwa AfrikaWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiLakabuTungo sentensiUhifadhi wa fasihi simuliziMizimu🡆 More