Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo: Nchi ya Afrika ya Kati

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (au Kongo-Kinshasa) ni nchi iliyoko Afrika ya Kati; kwa ukubwa wa eneo ni ya pili barani Afrika.

Ni tofauti na nchi jirani ya Jamhuri ya Kongo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo: Jiografia, Historia, Mikoa
Ramani ya Jamhuri.

Jiografia

Nchi imepakana na Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi, Tanzania, Zambia na Angola.

Ina sehemu ndogo ya pwani kwenye Bahari ya Atlantiki. Sehemu hiyo inatenganisha eneo la Cabinda kutoka maeneo mengine ya Jamhuri ya Angola.

Eneo lote ni la kilometa mraba 2,345,409 na linafanya Kongo iwe nchi ya 11 duniani kwa ukubwa wa eneo.

Historia

Historia ya kale

Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo: Jiografia, Historia, Mikoa 
Ufalme wa Kongo mnamo mwaka 1700

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani na ya Wabilikimo.

Katika karne za BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Jina la Kongo lahusiana na mto Kongo unaopitia nchi yote.

Mnamo karne ya 15, wakati wapelelezi wa kwanza Wareno walipofika kwenye pwani za Afrika, milki kubwa katika nchi ya Kongo ya magharibi pamoja na Angola ya kaskazini ilikuwa Ufalme wa Kongo. Wakati wa uenezaji mkuu ufalme huu ulianza kwenye mwambao wa Atlantiki na kuendelea hadi mto Kwango kwenye mashariki, halafu maeneo kutoka Pointe-Noire (leo: Jamhuri ya Kongo, upande wa kaskazini ya Cabinda) upande wa kaskazini hadi mto Loje (leo: mji wa Ambriz) katika kusini.

Mtawala alikuwa na cheo cha Manikongo na ufalme uligawiwa kwa majimbo sita. Baada ya kufika kwa Wareno wafalme na matabaka ya juu walikuwa Wakristo. Ufalme uliporomoka kutokana na vita vilivyosababishwa na biashara ya watumwa na kuingilia kwa wafanyabiashara ya watumwa katika siasa ya ndani. Hata hivyo, nasaba za watawala waliotumia cheo cha "Awenekongo" waliendelea kukaa katika mji mkuu wa kale M'banza-Kongo (iliyobadilishwa jina kuitwa San Salvador) hadi mwaka 1914 ambako Wareno walifuta mabaki ya uhuru na kufanya eneo lililobaki sehemu kamili ya koloni lao la Angola.

Upande wa kusini, kuanzia karne ya 17, kulikuwa na ufalme ulioitwa Dola la Kazembe.

Koloni binafsi la mfalme kuwa koloni la Ubelgiji

Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo: Jiografia, Historia, Mikoa 
Picha za watoto waliokatwa mikono kama adhabu chini ya Leopold II zilienea na kusababisha madai ya kumwondolea utawala wa Kongo.

Nchi jinsi ilivyo ilianzishwa kama Dola huru la Kongo likiwa mali binafsi ya mfalme Leopold II wa Ubelgiji. Historia yake ni ya aibu na ya ukatili kupindukia.

Utawala wa mfalme ulionekana kuwa wa kinyama na upinzani dhidi yake ulikua katika nchi nyingi za dunia.

Hatimaye alipaswa kukabidhi koloni lake binafsi mikononi mwa serikali ya Ubelgiji iliyomlipa fidia kwa mali aliyoacha.

Kati ya mwaka 1908 hadi 1960 ilikuwa koloni la Ubelgiji kwa jina la Kongo ya Kibelgiji baada ya kuhamishiwa mikononi mwa serikali ya Ubelgiji.

Katika miaka 1925 hadi 1946 maeneo ya Rwanda na Burundi yalitawaliwa kama sehemu za Kongo ya Kibelgiji.

Siasa ya wakoloni

Wabelgiji walijitahidi kuboresha hali ya maisha ya wenyeji baada ya miaka mibaya ya Leopold II. Nia ilichelewa kuonekana hali halisi kwa sababu utaratibu wa kulazimisha Waafrika kufanyia kazi kampuni na shirika kubwa iliendelea hata bila idhini ya serikali mpya ukadai vifo vingi.

Kwenye uwanja wa elimu, matibabu na mawasiliano jitihada za siasa mpya zilionekana zaidi. Kongo ilikuwa kati ya nchi chache ambako lugha za kienyeji zilifundishwa shuleni kwa sababu shule nyingi ziliendshwa na wamisionari.

Kwa upande mwingine ubaguzi wa rangi uliwaruhusu Waafrika wachache sana kufikia ngazi za juu za elimu.

Makampuni makubwa ya migodi kama vile "Société Générale" na "Union Minière du Haut Katanga" yalichimba madini hasa katika jimbo la Katanga. Makampuni haya yalikuwa na athira kubwa.

Katanga ilikuwa maarufu kwa shaba iliyochimbwa huko. halafu pia kwa uranium iliyotumiwa kwa mabomu ya kwanza ya kinyuklia ya Marekani mwaka 1945.

Upinzani

Baada ya unyama wa miaka ya Leopold II upinzani dhidi ya utawala wa kikoloni ulikuwa hafifu. Kuanzia miaka ya 1920 Wakongo wengi walionyesha upinzani huo katika mahudhurio katika madhehebu mapya ya wafuasi wa Simon Kimbangu yaliyopigwa marufuku na Wabelgiji kuanzia mwaka 1926.

Tangu mwaka 1950 upinzani uliongezeka na kuonyesha pia uso wa kisiasa.

Wabelgiji ambao hawakujiandaa kwa madai hayo yalipaswa kukubali uchaguzi wa halmashauri za vijiji na miji mwaka 1957.

Mwaka 1958 vyama vya kisiasa vilikubaliwa. Harakati mbili muhimu kati ya hivi zilikuwa Abako (Alliance de Bakongo) chini ya Joseph Kasavubu na MNC (Mouvement National Congolais) chini ya Patrice Lumumba.

Mwaka 1959 mkutano wa wanasiasa Wakongo ulidai uhuru wa nchi.

Mwisho wa koloni na uhuru

Wabelgiji walijaribu kuchelewesha harakati hizo lakini baada ya kutambua matatizo serikali ya Ubelgiji ilitangaza mnamo Januari 1960 kuwa uchaguzi utaendeshwa haraka na baada ya miezi sita Wabelgiji watakabidhi nchi kwa wenyeji.

Chama cha Patrice Lumumba kilishinda kwa kura nyingi naye akawa kiongozi wa kwanza wa nchi huru kama waziri mkuu.

Koloni la Kongo ya Kibelgiji lilipata uhuru tarehe 30 Juni 1960.

Kati ya 27 Oktoba 1971 na 17 Mei 1997, chini ya utawala wa dikteta Mobutu, nchi ilijulikana kwa jina la "Zaire".

Leo hii ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mikoa

Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo: Jiografia, Historia, Mikoa 
Mikoa 25 na mji mkuu Kinshasa.


Nchi imegawiwa katika mikoa 26 kadiri ya Katiba mpya (2006) na utekelezaji wake wa mwaka 2015.

Mkoa Mji Mkuu
1. Kinshasa Kinshasa
2. Kongo Kati   Matadi
3. Kwango Kenge
4. Kwilu Kikwit
5. Mai-Ndombe Inongo
6. Kasaï Luebo
7. Lulua Kananga
8. Kasaï Mashariki Mbuji-Mayi
9. Lomami Kabinda
10. Sankuru Lodja
11. Maniema Kindu
12. Kivu Kusini Bukavu
13. Kivu Kaskazini Goma
Mkoa Mji Mkuu
14. Ituri Bunia
15. Wele Juu Isiro
16. Tshopo Kisangani
17. Wele Chini Buta
18. Ubangi Kaskazini Gbadolite
19. Mongala Lisala
20. Ubangi Kusini Gemena
21. Équateur Mbandaka
22. Tshuapa Boende
23. Tanganyika Kalemie
24. Lomami Juu Kamina
25. Lualaba Kolwezi
26. Katanga Juu    Lubumbashi

Watu

Mwaka 2017 wakazi walikuwa 81,339,988: idadi hiyo ni ya 4 kati ya nchi zote za Afrika, baada ya Nigeria, Ethiopia na Misri.

Wakazi asilia ni Wabilikimo, ambao kwa sasa ni 600,000. Kumbe walio wengi ni Wabantu.

Lugha

Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo: Jiografia, Historia, Mikoa 
Maeneo ya lugha kuu za Kongo

Kifaransa ni lugha rasmi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ilikuwa lugha ya utawala ya koloni ikaendelea kutumiwa kama lugha isiyoelekea upande wowote kati ya makabila, lugha na tamaduni za nchi hii.

Lugha ya Kiholanzi iliyotumiwa na Wabelgiji pamoja na Kifaransa katika utawala haitumiki tena.

Kwa jumla kuna takriban lugha 242, hasa lugha za Kibantu, zinazozungumzwa nchini (angalia orodha ya lugha). Kati yake, lugha 4 zinatambuliwa kama lugha za kitaifa, nazo ni: Kikongo (Kituba), Kingala (Kongo), Kiluba (Tshiluba) na Kiswahili. Wakati wa ukoloni lugha hizo nne za kitaifa ziliwahi kutumiwa kieneo katika shule za msingi.

Kingala kilikuwa lugha rasmi ya jeshi la kikoloni lililoitwa "Force Publique" chini ya utawala wa Ubelgiji likaendelea kuwa lugha ya jeshi la jamhuri baada ya uhuru.

Tangu mapinduzi ya 1997 sehemu za jeshi, hasa mashariki, hutumia pia Kiswahili.

Takriban 47% wanatumia Kifaransa kama lugha ya kwanza au lugha ya pili.

Dini

Wananchi wengi (zaidi ya 90%) wanajihesabu Wakristo wa madhehebu mbalimbali; kati yao asilimia 29.7 ni Wakatoliki. Waislamu ni asilimia 10-12. Wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 3%.

Tazama pia

Marejeo

  • Osman, Mohamed Omer Guudle(November,2011) Africa: A rich Continent where poorest people live, The Case of DR Congo and the exploitation of the World Market

Viungo vya nje

Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo: Jiografia, Historia, Mikoa 
WikiMedia Commons


Nchi za Afrika Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo: Jiografia, Historia, Mikoa 
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo: Jiografia, Historia, Mikoa  Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo JiografiaJamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo HistoriaJamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo MikoaJamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo WatuJamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo Tazama piaJamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo MarejeoJamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo Viungo vya njeJamhuri Ya Kidemokrasia Ya KongoAfrikaAfrika ya KatiBaraJamhuri ya Kongo

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Ligi ya Mabingwa AfrikaUsawa (hisabati)VivumishiElibariki Emmanuel KinguWahayaMjusi-kafiriUundaji wa manenoGhanaPaul MakondaNdovuIstanbulHistoria ya ZanzibarBunge la TanzaniaUkwapi na utaoDemokrasiaAzimio la ArushaChe GuevaraLilithMuungano wa Tanganyika na ZanzibarNahauSkeliMichezoJoseph Leonard HauleMkoa wa Unguja Mjini MagharibiFisiVivumishi ya kuulizaMapambano ya uhuru TanganyikaAustraliaOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaAmri KumiThamaniIsraeli ya KaleWabunge wa kuteuliwaTaswira katika fasihiUmemeVita vya KageraKisimaVisakaleMweziNdiziMtakatifu MarkoKiimboJohn Samwel MalecelaMwenge wa UhuruChakulaOrodha ya makabila ya TanzaniaFonolojiaUzazi wa mpango kwa njia asiliaZakayoUhindiSayansiUtandawaziAfrika ya MasharikiVitendawiliMwanamkeTanzaniaDuniaLigi ya Mabingwa UlayaOrodha ya nchi kufuatana na wakaziBiashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiTashbihaCleopa David MsuyaWabena (Tanzania)Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaUmoja wa AfrikaMusaSilabiUrenoMkoa wa ArushaNgonjeraLigi Kuu Uingereza (EPL)MethaliAnwaniOrodha ya viongozi🡆 More