Jabari ni kundinyota linalojulikana pia kwa jina lake la kimagharibi la Orion.
Ni moja ya makundinyota yanayotambuliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia
Nyota za Jabari huwa hazipo pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisia kuna umbali mkubwa kati yake, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Jabari" linaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoliona kutoka duniani.
Jina la Kiswahili ni Jabari na linatokana na Kiarabu الجبار al-jabbaar ambalo linamaanisha "jitu". Jina hili lilipokewa na Waarabu kutoka kwa Waaramu waliosema gabbara "jitu". Wote walimaanisha hapa tabia ya mwindaji mkuu na nusu-mungu katika mitholojia ya Kigiriki aliyeitwa Ὠρίων orion na hivyo alitajwa katika kitabu cha Almagesti cha Klaudio Ptolemaio.
Jabari ni kati ya makundinyota yanayoonekana vyema kwenye angakusi na pia angakaskazi ya Dunia. Nyota saba angavu sana zinakumbukwa kirahisi na watazamaji wa anga.
Nyota nne za Rijili ya Jabari (Rigel), Ibuti la Jauza (Betelgeuse), Bellatrix and Saiph zinafanya pembenne, na katikati kuna safu ya nyota tatu za karibu zinazoitwa "ukanda" ambazo ni Alnitak, Alnilam na Mintaka (ζ, ε na δ Orionis). Chini ya nyota za ukanda kuna nyota angavu inayotambuliwa kwa darubini ndogo kuwa nebula angavu, hii ni Nebula ya Jabari (Orion nebula).
Jina la (Bayer) | Namba ya Flamsteed | Jina (UKIA) | Mwangaza unaoonekana | Umbali (miakanuru) | Aina ya spektra |
---|---|---|---|---|---|
α | 58 | Ibuti la Jauza - Betelgeuse | 0,0 bis 1,3m | 640 | M1-2 Ia-Iab |
β | 19 | Rijili ya Jabari - Rigel | 0,03 bis 0,3m | 773 | B8 Iab + B9 V + B9 V |
γ | 24 | Bellatrix | 1,64m | 243 | B2 III |
ε | 46 | Alnilam | 1,69m | 1342 | B0 Iab |
ζ | 50 | Alnitak | 1,74m | 818 | O9.7 Ibe + O + B0 III |
κ | 53 | Saiph | 2,07m | 722 | B0.5 Iavar |
δ | 34 | Mintaka | 2,20 bis 2,35m | 916 | O9.5 II + B2 V |
ι | 44 | Hatysa | 2,75m | 1326 | O9 III |
π3 | 1 | Tabit | 3,19m | 26 | F6 V |
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jabari kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Jabari, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.