Australia: Nchi katika Oceania

Australia ni bara pia ni nchi huru ya Oceania.

Ikiwa na eneo la km² 7,617,930 ni bara dogo kuliko yote duniani, na ni kisiwa kikubwa kuliko vyote. Kama nchi ni ya sita kwa ukubwa.

Australia

Iko kusini kwa Indonesia na Papua Guinea Mpya na iko magharibi kwa New Zealand. Mara nyingi visiwa vya New Zealand huhesabiwa kuwa sehemu ya bara la Australia. Vilevile Australia huangaliwa pamoja na visiwa vya Pasifiki katika orodha ya mabara ya dunia kama "Australia na Pasifiki".

Idadi ya wakazi ni 25,970,200 (mwaka 2022).

Jiografia

Australia: Jiografia, Ekolojia, Historia 
Hali ya hewa Australia kufuatana na Köppen classification.

Bara la Australia linakaa juu ya sehemu imara ya bamba la Australia bila mipaka ya gandunia na kwa hiyo hakuna volkeno; matetemeko ya ardhi ni madogo tu.

Umbali kati ya magharibi na mashariki ni km 4,000, na kati ya kaskazini na kusini umbali ni km 3,700.

Australia huzungukwa na bahari ya Hindi, bahari ya Pasifiki na Bahari ya Kusini. Kwa jumla ina pwani yenye urefu wa kilomita 34,218.

Great Barrier Reef mbele ya pwani ya mashariki-kaskazini ni vipwa vya matumbawe vikubwa duniani; ina urefu wa kilomita 2,000.

Sehemu kubwa ya bara ni jangwa au maeneo yabisi sana. Takriban asilimia 40 ya eneo limefunikwa na matuta ya mchanga. Ardhi yenye rutuba iko kusini-mashariki na kona ya kusini-magharibi pamoja na hali ya hewa isiyo na joto kali. Hali ya hewa kaskazini ni ya kitropiki na huko kuna misitu minene pamoja na savana na jangwa.

Sehemu kubwa ya uso wa nchi ni tambarare na majangwa. Kwenye pwani ya mashariki na pia upande wa magharibi kuna safu za milima inayopanda hadi kimo cha mita 2,200. Sehemu ya juu kabisa huitwa milima ya theluji au Alpi za Australia na mlima Kosciuszko unafikia kimo cha mita 2,229. Huko kuna barafuto za kudumu.

Sehemu ya chini iko kwenye beseni la ziwa Eyre iliyopo mita 17 chini ya usawa wa bahari. Tako la beseni hilo mara nyingi ni kavu kabisa, huwa pamejaa maji mara chache tu baada ya mvua kubwa sana.

Mahali pakavu kabisa ni jangwa la Simpson lenye usimbishaji chini ya 200 mm kwa mwaka.

Mito muhimu inaanza katika Alpi za Australia: ni Murray na Darling inayomwagilia beseni la Murray-Darling na hii ni eneo muhimu la kilimo cha Australia.

Mingine ni Mto Snowy na Mto Murrumbidgee, halafu mto Fitzroy (Queensland), mto Ord, mto Swan (Australia ya Magharibi), mto Derwent, mto Tamar (Tasmania) na mto Hawkesbury (New South Wales).

Sehemu kubwa ya bara haina watu. Wakazi wengi pamoja na miji yote wako kwenye pwani ya mashariki na kusini.

Miji mikubwa ni Sydney (wakazi milioni 3.7), Melbourne (wakazi milioni 3.6), Brisbane (wakazi milioni 1.7), Perth (wakazi milioni 1.4) na Adelaide (wakazi milioni 1.1).

Mji mkuu, Canberra (wakazi 308,700), ulijengwa kati ya Sydney na Melbourne kwa sababu miji hiyo miwili ilishindwa kukubaliana ni upi unaostahili kuwa mji mkuu.

Uchumi katika maeneo yabisi ni hasa ufugaji wa kondoo milioni 130 na ng'ombe milioni 25.

Ekolojia

Australia ilitengana na mabara mengine miaka milioni mingi iliyopita. Kwa sababu hiyo kuna aina nyingi za pekee za mimea na wanyama zisizopatikana penginepo duniani. Wanyama wa pekee ni kwa mfano kanguru na koala. Miti ya Australia kama vile mkalitusi imepelekwa kote duniani katika nchi zenye hali ya hewa ya kufaa.

Historia

Watu wa kwanza walifika Australia takriban miaka 65,000 iliyopita. Walitunza utamaduni wa wawindaji-wakusanyaji hadi kufika kwa wakoloni (1606).

Hakuna habari kama watu wa Asia walifikia Australia lakini tangu karne ya 17 BK Waholanzi halafu Waingereza walifika kwa jahazi zao.

Australia ikawa mahali pa koloni la kigereza na wafungwa kutoka Uingereza walipelekwa huko katika karne ya 19. Baadaye walifika pia walowezi huru.

Idadi ya Waustralia asilia imepungua sana kutokana na magonjwa mapya wakiambukizwa na Wazungu, pia walitendewa vibaya na kufukuzwa katika sehemu kubwa ya nchi yao.

Australia ilipata uhuru wake mwaka 1901 lakini inaendelea kumkubali malkia ya Uingereza kama Mkuu wa Dola akiwasilishwa na Gavana Mkuu. Mamlaka imo mikononi mwa waziri mkuu na serikali yake.

Serikali

Muundo wa utawala ni wa shirikisho. Kuna majimbo 6 ya kujitawala pamoja na maeneo ambayo yako moja kwa moja chini ya serikali ya shirikisho.

Lugha

Australia haina lugha rasmi, lakini 72% ya wakazi nyumbani wanaongea Kiingereza cha Kiaustralia tu. Lugha nyingine zinazotumika na zaidi ya 1% ya wakazi ni ni Kichina, Kiarabu, Kivietnam, Kipanjabi n.k. Wachache nyumbani wanaongea mojawapo kati ya lugha asili za Australia. Angalia pia Orodha ya lugha za Australia.

Dini

Katika sensa ya mwaka 2021, Wakristo walikuwa 43.9% ya wakazi wote, wakiongozwa na Wakatoliki (20%) na Waanglikana (9.8). Waislamu walikuwa 3.2%, Mabanyani 2.7%, Wabuddha 2.4%, Singasinga 0.8%, Wayahudi 0.4% n.k. 38.9% walisema hawana dini yoyote.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje


Australia: Jiografia, Ekolojia, Historia  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Tags:

Australia JiografiaAustralia EkolojiaAustralia HistoriaAustralia SerikaliAustralia LughaAustralia DiniAustralia Tazama piaAustralia TanbihiAustralia MarejeoAustralia Marejeo mengineAustralia Viungo vya njeAustraliaBaraDunianiKisiwaKm²Nchi huruOceania

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Uhakiki wa fasihi simuliziUundaji wa manenoMaji kujaa na kupwaMbwana SamattaBahari ya HindiJackie ChanBaraza la mawaziri TanzaniaLigi ya Mabingwa AfrikaMichael JacksonKalenda ya KiislamuHistoria ya WasanguArsenal FCSiafuIdi AminNgw'anamalundiSamakiUnyanyasaji wa kijinsiaNgome ya YesuSemiMaumivu ya kiunoSabatoBahari ya ShamuElimuEthiopiaManchester CityAntibiotikiKitomeoMaji ya chumviMfumo wa upumuajiWanyakyusaMtume YohaneTovutiIjumaa KuuVidonge vya majiraVitenzi vishiriki vipungufuUtamaduniKamusi ya Kiswahili sanifuInjili ya MathayoVivumishi vya sifaUmoja wa Muungano wa AfrikaPunyetoWajitaSkeliAustraliaBob MarleyBikiraUaJohn MagufuliNominoTwigaMbuFalsafaAlfabetiHistoria ya AfrikaOsama bin LadenNahauMafarisayoMaadiliJakaya KikweteTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaMkanda wa jeshiJumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta dunianiWamandinkaAli ibn Abu TalibUfufuko wa YesuSanaa za maoneshoKitenzi kikuu kisaidiziDakuMkoa wa SingidaJumamosi kuuMapambano kati ya Israeli na PalestinaKiwakilishi nafsiMavaziMnyama🡆 More