Filamu 1997 Titanic

Titanic ni filamu ya kusikitisha na ya mapenzi inayohusu kuzama kwa meli ya Titanic.

Filamu hii iliongozwa, ikaandikwa, ikatayarishwa na kuhaririwa na James Cameron mnamo 1997. Wahusika wake ni Leonardo DiCaprio kama Jack Dawson na Kate Winslet kama Rose DeWitt Bukater. Wawili hawa wenye maisha tofauti walipendana pindi walipokutana kwenye meli hii ambayo haikuwa na mwisho mwema.

Titanic
Filamu 1997 Titanic
Picha ya filamu ya Titanic
Aina Mchezo wa mapenzi, Picha ya Kusikitisha
Imetungwa na James Cameron
Imeongozwa James Cameron
Nchi inayotoka Marekani
Lugha Kiingereza
Utayarishaji
Watayarishaji
wakuu
James Cameron
Jon Landau
Muda makisio ni dk. 194
Urushaji wa matangazo
Kituo 20th Century Fox
Inarushwa na 19 Desemba 1997

Filamu hii ilikuwa itolewe mnamo 2 Julai 1997 lakini tarehe ikapelekwa mbele hadi 19 Desemba 1997. Filamu hii ilipata mafanikio makubwa, kwa kushinda tuzo kumi na moja za Academy Awards.

Kuhusu "Titanic"

Mnamo 1912, Rose DeWitt Bukater (Kate Winslet) aliye na miaka kumi na saba anaingia kwenye meli mjini Southampton pamoja na mchumba wake aitwaye Caledon "Cal" Hockley (Billy Zane), tajiri mmoja aliye na miaka thelathini na mamake - Ruth DeWitt Bukater (Frances Fisher). Cal na Ruth wanasisitiza kuhusu sherehe ya uchumba wa Rose, kwani kuoana kwao kutatoa madeni yote ambayo familia ya DeWitt Bukater wanayo. Rose anataka kujiuwa kwa kujirusha baharini kutokamana na kulazimishwa kuolewa na mtu asiyempenda. Kabla hajajirusha, mchoraji mmoja aitwaye Jack Dawson (Leonardo DiCaprio) anamzuia. Papo hapo, Cal na rafiki zake wanaskia kelele alizopiga Rose na wakifika hapo wanadhania kuwa Jack alikuwa anataka kumbaka Rose. Rose anawaelezea kuwa Jack ameokoa maisha yake, kwani aliteleza na karibu aanguke pindi Jack alimshikilia. Hakusema ukweli kuwa alikuwa anataka kujiuwa. Jack na Rose wanaanza kuwa marafiki.

Filamu 1997 Titanic 
Picha hii ya Rose akiwa tupu ilichorwa na James Cameron

Jack anamchukua Rose kwenye sherehe iliyofanyika kwenye daraja la tatu. Cal alipopata habari, alimkataza Rose kuonana na Jack tena. Rose anakataa, na anamfuata Jack, akiona kuwa afadhali awe na Jack kuliko Cal. Jack na Rose wanaingia chumbani halafu Rose anamwambia Jack amchore akiwa uchi. Baada ya hapo, wawili hao wanafanya kitendo cha mapenzi. Papo hapo, meli hii inagonga jiwe laa barafu. Cal anaiona hiyo picha ya Rose, na kwa hasira, anatoa amri kwa askari wamshike na kumsingizia kuwa ameiba. Jack anafungwa pingu kwenye chuma ili asiweze kukimbia. Rose akatafuta panga na akavunja hizo pingu na kumfungua Jack. Meli inaanza kuvuja na kuzama.

Filamu 1997 Titanic 
Meli ya Titanic ikizama.

Cal anamhimiza Rose apande dau ndogo itakayomuokoa. Rose anakubali lakini shingo upande. Mwishowe, alishuka kwenye dau na kurudi kwenye meli na kukumbatiana na mpenzi wake - Jack.Meli inapozama, Jack anatafuta kipande cha mbao watakacholalia ili wasizame. Kwa bahati mbaya, Jack anapata kipande kidogo cha kumtosheleza Rose pekee yake. Pindi waokoaji walivyokuja, Rose alimwamsha Jack lakini alikuwa amefariki kwa ajili ya maji yalivyokuwa baridi sana.

Wahusika Wakuu

  • Leonardo DiCaprio aliigiza kama Jack Dawson. Kwenye filamu hii, Jack ni mtu maskini hohe hahe. Anacheza mchezo wa kamari na kushinda tiketi ya kuingia kwenye meli ya Titanic. Anapendana na msichana wa kitajiri aitwaye Rose DeWitt.
  • Kate Winslet aliigiza kama Rose DeWitt, ambaye ni msichana wa miaka kumi na saba aliyeposwa na jibaba tajiri la miaka takriban thelathini. Kate alimwacha tajiri na kupendana na Jack, aliye maskini hohehahe.
  • Billy Zane aliigiza kama Caledon "Cal" Hockley ambaye ni mwanamume tajiri aliyetaka kumuoa Rose.
  • Frances Fisher aliigiza kama Ruth DeWitt ambaye ni mamake Rose. Ruth ndiye aliyepanga uchumba wa Rose na Cal.
  • Danny Nucci aliigiza kama FabrizioDe Rossi ambaye ni rafikiye Jack.

Wimbo wake

Wimbo wake ulitungwa na James Horner. Wimbo huo wa "My Heart Will Go On" uliimbwa na Celine Dion.

Tuzo

  • Titanic ilishinda tuzo nne za Golden Globe za Best Motion Picture, Best Director, Best Original Score na Best Song.
  • Ilishinda tuzo 11 kutoka kwa Academy Awards.
  • Ilishinda tuzo tatu za Grammy Award: Record of the Year, Song of the Year na Best Song Written for a Motion Picture.
  • "My Heart Will Go On" ilishinda tuzo la Grammy Award ("Best Song Written Specifically for a Motion Picture or for Television").
  • Hatimaye, Titanic ilishinda tuzo takriban 90 kote duniani.

Marejeo

Viungo vya nje

Tags:

Filamu 1997 Titanic Kuhusu TitanicFilamu 1997 Titanic Wahusika WakuuFilamu 1997 Titanic Wimbo wakeFilamu 1997 Titanic TuzoFilamu 1997 Titanic MarejeoFilamu 1997 Titanic Viungo vya njeFilamu 1997 TitanicLeonardo DiCaprioMeliTitanic

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KataOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaBabuFasihi simuliziMwanzoKisononoStadi za lughaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoVirusi vya UKIMWIUkoloniAkiliAjuzaKamusi ya Kiswahili sanifuBikiraLilithVivumishi ya kuulizaMkondo wa umemeMalariaUkimwiWahangazaMkonoKamusi za KiswahiliMbuyuMkoa wa SongweMfumo wa mzunguko wa damuNyumbaFonimuTabianchiVita Kuu ya Kwanza ya DuniaLahaja za KiswahiliTashbihaVielezi vya mahaliMizimuHifadhi ya SerengetiAslay Isihaka NassoroUkristoMatiniMwanzo (Biblia)Kiwakilishi nafsiMisimu (lugha)Bendera ya TanzaniaMbuniUjimaRwandaShabuSarufiWasukumaKibodiJoyce Lazaro NdalichakoRitifaaUharibifu wa mazingiraKitenziJumuiya ya MadolaVitenzi vishiriki vipungufuChe GuevaraMafua ya kawaidaWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiKinjikitile NgwaleKilatiniDawatiUNICEFLatitudoReal MadridGeorge WashingtonAbedi Amani KarumeNomino za dhahaniaUkabailaHoma ya matumboMkoa wa NjombeUkristo barani AfrikaKontuaUandishi wa inshaUfinyanziStashahada🡆 More