Roald Engebreth Gravning Amundsen (Borge, leo: Fredrikstad, Norwei, 16 Julai 1872 - Aktiki, mnamo 18 Juni 1928) alikuwa mpelelezi Mnorwei aliyekuwa mtu wa kwanza kufika Ncha ya kusini mwaka 1911.
Kabla ya hapo alikuwa mtu wa kwanza aliyefaulu kuvuka mapito ya kaskazini-magharibi kati ya Atlantiki na Pasifiki katika miaka 1903 - 1906.
Katika safari mbalimbali alikuwa pia mtu wa kwanza aliyevuka Aktiki na ncha ya kaskazini hewani kwa kutumia ndegeputo mwaka 1926.
Alikufa mwaka 1928 kwenye Aktiki alipojaribu kumwokoa mpelelezi Mwitalia aliyekuwa amepotea katika barafu.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Roald Amundsen, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.