Malta: Jimbo kuu la Kusini mwa Ulaya lililo kwenye visiwa katika Bahari ya Mediterania

Malta ni nchi ndogo kwenye funguvisiwa katikati ya bahari ya Mediteranea.

Malta
Malta: Jiografia, Miji, Historia
Ramani ya Malta
Malta: Jiografia, Miji, Historia
Malta kutoka angani

Malta iko km 93 kusini kwa kisiwa cha Sisilia (Italia), upande wa mashariki kwa Tunisia na kaskazini kwa Libya.

Jiografia

Funguvisiwa la Malta lina visiwa saba. Visiwa vikubwa viwili ni Malta (km² 246) na Gozo (km² 70). Kuna kisiwa cha tatu kinachokaliwa na watu, ndicho Comino (km² 3). Vingine ni vidogo, havina watu. Jumla la eneo ni km² 316.

Visiwa vya Malta ni mabaki ya kanda la nchi kavu lililokuwa linaunganisha Afrika na Ulaya na lililokatwa na kupanda kwa usawa wa bahari tangu mwaka 11000 KK hivi.

Malta: Jiografia, Miji, Historia 
Pwani ya Mellieħa Bay.

Sehemu za juu ni vilima vya Dingli Cliffs vyenye kimo cha mita 245 juu ya UB.

Tatizo kubwa la Malta ni uhaba wa maji baridi. Siku hizi vituo vinne vya kuondoa chumvi kwenye maji ya bahari kwa njia ya osmosi vinatengeneza maji ya kunywa. Maji machafu husafishwa na mvua kukusanywa.

Miji

Malta: Jiografia, Miji, Historia 
Valletta.

Miji mikubwa zaidi ni: St. Paul's Bay (29,097), Birkirkara (wakazi 21,676), Qormi (wakazi 18,230), Mosta (wakazi 17,789), Zabbar (wakazi 15,030), Victoria (wakazi 12,914) na San Gwann (wakazi 12,346).

Mji mkuu, Valletta, una wakazi 7,173 tu.

Historia

Malta ilikaliwa na watu tangu milenia ya 4 KK. Kuna magofu ya hekalu la mwaka 3200 KK hivi.

Baadaye funguvisiwa lilitawaliwa na Wafinisia, Karthago na Dola la Roma.

Malta inatajwa katika Biblia kwa sababu Mtume Paulo aliponea huko baada ya kuzama kwa merikebu alimosafiri baharini kuelekea Roma (Mdo 27:39 n.k.).

Waarabu walivamia visiwa hivyo mwaka 870 na kuvitawala hadi 1091.

Baadaye vilitawaliwa na Wanormandi wa Italia Kusini, halafu na Wahispania chini ya mamlaka ya Dola Takatifu la Kiroma la Ujerumani.

Tangu mwaka 1530 visiwa vilikabidhiwa na Kaisari kwa askari wa Vita vya msalaba wa Chama cha Wanahospitali wa Mt. Yohane wa Yerusalemu.

Wanamisalaba hao walitawala visiwa hivyo hadi Napoleoni alipoteka Malta mwaka 1799 akiwa safarini kwenda Misri.

Uingereza ulitwaa visiwa kutoka kwa Ufaransa ukatawala Malta hadi uhuru wake tarehe 21 Septemba 1964.

Tarehe 13 Desemba 1974 Malta ikatangazwa kuwa jamhuri ndani ya Jumuiya ya Madola.

Tarehe 1 Mei 2004 nchi ikajiunga na Umoja wa Ulaya.

Watu

Kwa jumla kuna wakazi 404,039: wa kiume 200,715 (49.7%) na wa kike 203,324 (50.3%). Msongamano wa watu ni 1,282 kwa kilomita ya mraba ambao ni msongamano mkubwa kati ya nchi zote za Ulaya. Katika karne ya 21 nchi imepokwa wahamiaji wengi, ambao kwa sasa ni 23.17% za wakazi wote.

Lugha ya Kimalta ni lugha ya pekee. Asili yake ni lahaja ya Kiarabu iliyopokea maneno mengi ya Kiitalia, Kisisili, Kiingereza, Kihispania na Kifaransa. Ni lugha pekee ya Kisemiti inayoandikwa rasmi kwa alfabeti ya Kilatini.

Lugha rasmi ya pili ni Kiingereza kutokana na miaka 150 ya ukoloni wa Uingereza. Wamalta wengi sana (66%) huelewa pia lugha ya nchi kubwa jirani, Italia.

wakazi wengi (90%) ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (83%), ambalo imani yake ndiyo dini rasmi ya nchi. Waislamu ni asilimia 2.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Malta: Jiografia, Miji, Historia 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Serikali
    Taarifa za jumla
    Vyombo vya habari
    Safari


Nchi za Umoja wa Ulaya Malta: Jiografia, Miji, Historia 
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Malta: Jiografia, Miji, Historia  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Malta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Malta JiografiaMalta MijiMalta HistoriaMalta WatuMalta Tazama piaMalta TanbihiMalta MarejeoMalta Viungo vya njeMaltaBahariFunguvisiwaMediteranea

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MjasiriamaliTanganyika (ziwa)Orodha ya mito nchini TanzaniaMohamed HusseinWhatsAppSaidi NtibazonkizaMwakaUsawa bahari wastaniAli ibn Abu TalibNdoa katika UislamuChadLughaMpira wa kikapuMsitu wa AmazonKisononoOrodha ya wanamuziki wa hip hopMaambukizi ya njia za mkojoVivumishi vya sifaHoma ya matumboAzimio la kaziTashihisiJiniShuleEe Mungu Nguvu YetuUmoja wa Muungano wa AfrikaSerikaliKonsonantiDini nchini TanzaniaJamhuri ya Watu wa ChinaJuma NatureKomaChuma barani AfrikaSteven KanumbaMjombaHoma ya dengiDiamond PlatnumzAgano JipyaDr. Ellie V.DAlhamisi kuuBiblia ya KikristoJackie ChanMaumivu ya kiunoMtiNomino za jumlaWiki FoundationUnyevuangaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaUsimbajiBusaraTanzaniaOrodha ya Marais wa UgandaNgeli za nominoSheriaWanyama wa nyumbaniTaasisi ya Taaluma za KiswahiliUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaWikipediaBob MarleyMandhariNathariAfrikaUzazi wa mpango kwa njia asiliaMohammed Gulam DewjiJohn MagufuliPasifikiFasihi simuliziMsalabaMorokoMpira wa miguuMaudhuiUzazi wa mpangoOrodha ya miji ya TanzaniaNgonjeraMachweoJiografia ya Urusi🡆 More