Singapuri: Sinia

Singapuri ni nchi ndogo katika Asia ya Kusini-Mashariki.

Singapuri
Singapuri: Jiografia, Historia, Wakazi
Ramani ya Singapuri

Jiografia

Eneo lake ni kisiwa kwenye ncha ya kusini kabisa ya Rasi ya Malay pamoja na visiwa vidogo vya kando. Kisiwa kimetenganishwa na bara kwa mfereji mwembamba wa Johor.

Kuna mji mmoja tu: ni jiji la Singapuri lilipopo kisiwani, hivyo huhesabiwa pia kati ya dola-miji.

Historia

Kisiwa kiliwahi kuwa na makazi mbalimbali katika historia. Mji wa kisasa ulianzishwa mwaka 1819 na Waingereza kama kituo cha biashara ikawa bandari muhimu ya eneo.

Uingereza uliipa uhuru kama sehemu ya shirikisho la Malaysia. Lakini matatizo ya kuelewana yalionekana haraka kati ya wanasiasa Wamalay wa bara na wenzao Wachina wa kisiwani.

Mwishowe Singapuri ikafukuzwa katika shirikisho ikawa nchi ya kujitegemea tarehe 9 Agosti 1965. Mwanasiasa Lee Kuan Yew alikuwa waziri mkuu wa kwanza akaendelea na cheo hiki hadi mwaka 1990 akaongoza Singapuri kuwa kati ya mataifa matajiri ya Asia.

Wakazi

Kati ya wakazi milioni tano na nusu walio wengi (74.3%) ni wa asili ya China. Mababu wao walihamia huko wakitafuta kazi bandarini.

Wengine ni wakazi asilia Wamalay (13.5%) na Watamil na wengineo waliotokea Uhindi (9%).

Kuna lugha 24 ambazo huzungumzwa nchini Singapuri. Lugha rasmi ni Kiingereza (48.3%), Kichina (38.6%), Kimalay (9.2%) na Kitamil (2,5%).

Upande wa dini, 31.1% ni Wabuddha, 18.9% ni Wakristo, 15.6% ni Waislamu, 8.8% ni Watao, 5% ni Wahindu.

Uchumi

Uchumi wa Singapuri unategemea zaidi biashara, hasa benki pamoja na viwanda.

Imekuwa kitovu cha uchumi na biashara kwa Asia ya Kusini.

Tazama pia

Viungo vya nje

Singapuri: Jiografia, Historia, Wakazi 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Serikali
    Taarifa za jumla
    Biashara
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Singapuri: Jiografia, Historia, Wakazi  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Singapuri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Singapuri JiografiaSingapuri HistoriaSingapuri WakaziSingapuri UchumiSingapuri Tazama piaSingapuri Viungo vya njeSingapuriAsia ya Kusini-Mashariki

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

17 ApriliUkristoPichaKisononoWhatsAppMwigizajiWakingaBorussia DortmundUainishaji wa kisayansiSakramentiMkoa wa MbeyaMimba kuharibikaKima (mnyama)Everest (mlima)WikipediaMaambukizi nyemeleziBundiVitenzi vishirikishi vikamilifuWahayaMkoa wa ArushaBakari Nondo MwamnyetoMkanda wa jeshiYesuWajitaSaratani ya mlango wa kizaziSaidi NtibazonkizaFani (fasihi)Vivumishi ya kuulizaUmoja wa Muungano wa AfrikaMeno ya plastikiMisimu (lugha)Rupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniHistoria ya IranBawasiriOrodha ya shule nchini TanzaniaKombe la Mataifa ya AfrikaDhamiraInsha ya kisanaaKibwagizoTetekuwangaMaajabu ya duniaUaKiambishi tamatiElimuChuraUundaji wa manenoUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiPunyetoShambaKitenzi kikuuMshubiriUkoloni MamboleoMatiniSaudiaDoto Mashaka BitekoVivumishi vya kumilikiKiambishi awaliKamusi elezoBwehaLatitudoFonolojiaYoung Killer MsodokiUchumiMakabila ya IsraeliBahari ya HindiAngolaAgano la KaleNomino za dhahaniaIbadaMaji kujaa na kupwaUzalendoKidole cha kati cha kandoTiktok🡆 More