Simu

Simu (kutoka Kiarabu سیم, sim, inayomaanisha waya) ni kifaa cha elektroniki kinachotumiwa kwa mawasiliano ya mbali kwa kutumia sauti, ujumbe wa maandishi, au njia nyingine za kidigitali.

Simu
Simu ya zamani.
Simu
Simu ya mkononi.
Simu
Simu za kisasa.

Ina uwezo wa kupokea na kutuma taarifa kutoka sehemu mbalimbali kupitia mtandao wa mawasiliano, kama vile simu za mkononi au simu za mezani. Simu pia inaweza kuwa na huduma zingine kama kamera, kumbukumbu, na uwezo wa kupata mtandao wa intaneti, na hutumika kwa madhumuni mengi kama vile mawasiliano ya kibinafsi, kazi, au burudani.

Awali simu ilihitaji iunganishwe na nyaya, lakini leo hii inaweza kutumia redio. Hiyo inaitwa nyayatupu, siwaya au simu bila waya.

Historia

Watu wengi wanaamini kuwa simu iligunduliwa mnamo 1876 na Alexander Graham Bell, Mskoti mwenye umri wa miaka 29 aliyeishi nchini Marekani. Lakini Mwitalia Antonio Meucci alianzisha matumizi ya simu toka mwaka wa 1871 hukohuko Marekani.

Tangu mwishoni mwa karne ya 20 kuna aina mpya ya simu iliyoenea ambayo ni simu ya mkononi. Ingawa haistahili kweli kuitwa tena "simu" kwa maana asilia kwa sababu hakuna simu, ni aina ya mtambo wa mawasiliano uliosambaa haraka sana.

Katika nchi nyingi za Afrika simu hizi zina faida ya pekee kwa sababu zinaruhusu mawasiliano hata pale ambako nyaya za Posta hazifiki.

Namba za simu

Kila simu inapaswa kuwa na namba ya pekee ikiunganishwa katika mtandao wa simu. Isipokuwa ofisi au kampuni inaweza kuwa na namba moja kwa simu zake zote halafu maungio ya simu ya ndani ambako ama mtu au mtambo unaunganisha simu za ndani na mtandao wa nje.

Kwa kawaida mtandao wa simu ndani ya nchi inagawiwa kwa maeneo. Maeneo haya yanaweza kugawiwa tena hadi ngazi ya mtandao wa mahali. Kila eneo linafikiwa kupitia namba ya eneo; ndani ya eneo inatosha kutumia namba ya simu yenyewe.

Mfano: simu ya namba 556677 iko mjini Dar es Salaam. Namba ya eneo la Dar es Salaam ni 022. Kufikia simu hii ndani ya eneo la Dar es Salaam inatosha kupiga 556677. Mtu anayetaka kuipigia kutoka Dodoma au Arusha anatangulia namba ya eneo na kupiga 022-556677.

Simu za mkononi huunganishwa katika mtandao mkubwa wa kitaifa kufuatana na kampuni inayotoa huduma kama vile Airtel, TIGO au TTC yenye mtandao wake wa pekee. Kwa teknolojia bila waya hakuna haja ya ugawaji wa kieneo. Lakini kwenye simu hizi ni lazima kutumia pia namba ya mtandao muda wote. Kwa kupiga simu ya kawaida kutoka simu ya mkononi ni lazima kutumia muda wote namba ya kieneo hata kama mwenye kupiga yuko mji uleule maana mitandao ni tofauti.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Simu  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Simu HistoriaSimu Namba za simuSimu Tazama piaSimu MarejeoSimu Viungo vya njeSimuDijitiElektronikiKiarabuKifaaMaandishiMawasilianoSautiUjumbeWaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Homa ya manjanoLisheJulius NyerereEdward Ngoyai LowassaViunganishiLigi Kuu Tanzania BaraItikadiMichael JacksonUlemavuUajemiMhusika (fasihi)KaswendeUrenoWanyakyusaNambaMichezo ya jukwaaniWapogoloMohammed Gulam DewjiDodoma (mji)NeemaNyaniVielezi vya mahaliVivumishi vya kumilikiInjili ya MathayoSautiViwakilishi vya kumilikiUjamaaApril JacksonBunge la TanzaniaLuhaga Joelson MpinaMohamed HusseinJuxMazungumzoWachaggaMweziTanganyika (ziwa)Viwakilishi vya urejeshiMafurikoMvuaAdolf HitlerRitifaaLongitudoOrodha ya maziwa ya TanzaniaMunguRoho MtakatifuClatous ChamaSemantikiMgawanyo wa AfrikaMishipa ya damuHussein KaziOrodha ya kampuni za TanzaniaBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiUgonjwa wa uti wa mgongoLafudhiMshale (kundinyota)Taswira katika fasihiMtotoKampuniHifadhi ya Mlima KilimanjaroLingua frankaKadi ya adhabuHadithiNdoaPemba (kisiwa)UkabailaUyahudiMsokoto wa watoto wachangaAnthropolojiaMtakatifu PauloOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaFutiMkoa wa Kigoma🡆 More