Namba (au nambari) ni dhana na lugha inayotumiwa kutofautisha idadi au kupima kiwango.
Namba zinazojulikana zaidi ni zile namba asilia kama vile 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10 na kadhalika.
Utaalamu unaoshughulika habari za namba ni hasa hisabati pamoja na matumizi yote yake katika fani kama vile uhandisi, uchumi, takwimu na sayansi mbalimbali. Hisabati inatumia dhana ya "namba" kwa upana mkubwa hata nje ya namba asilia. Hisabati inajua
namba kamili (integer) zinazojumlisha namba asilia, sifuri na namba hasi. Namba hizi huandkiwa kirahisi kwa kutumia tarakimu (numerali) yaani alama zinazoweza kuonyesha namba.
namba wiano yaani kila namba inayoweza kuandikwa kwa umbo la sehemu kama vile , , , , na kadhalika au pia kuandikwa kwa mfumo desimali kama vile 4, 0.5, 0.04, 2.5 na kadhalika.
namba zisizowiana zisizolingana na sehemu, kwa mfano namba ya duara π (Pi) ambayo haiwezi kuandikwa kikamilifu kwa kutumia tarakimu.
namba halisi zinazojumlisha namba kamili, namba wiano na namba zisizowiani, yaani namba zote ambazo zingeweza kutokea katika mstari endelevu.
namba changamano ambazo zina sehemu mbili, ya kwanza ni namba halisi, na ya pili ni namba inayofikiriwa tu.
namba tasa zisizogawiwa kwa namba nyingine isipokuwa kwa 1 na kwa namba yenyewe.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Namba, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses. ®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.