A ni herufi ya kwanza katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa.
Alfabeti ya Kilatini (kwa matumizi ya Kiswahili) | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Aa | Bb | Cc | ch | Dd | ||
Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj | |
Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp | |
Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | ||
Ww | Xx | Yy | Zz |
Kichwa ch ng'ombe (Alama ya kale iliyokuwa silabi) | "Alef" ya Wafinisia (neno lao kwa ng'ombe) | Kigiriki Alfa | Kilatini A |
---|---|---|---|
Asili ya herufi A ni miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.
Kama herufi nyingine za alfabeti ya Kigiriki alfa imetoka katika alfabeti ya Wafinisia iliyokuwa alfabeti ya kwanza ya dunia. Wafinisia waliendeleza mwandiko wa kikabari wa kale uliokuwa mwandiko wa silabi na kuifanya alfabeti ya herufi moja-moja.
Faida ya alfabeti ni ya kwamba inahitaji alama chache kulingana na mwandiko wa silabi mwenye alama kwa kila silabi ya lugha fulani au mwandiko picha unaohitaji maelfu ya alama za picha.
Wafinisia walichukua alama ya ng'ombe wakairahisisha na kuiita kwa neno lao "alef" lenye maana ya "ng'ombe" lakini walisoma tu "'" yaani kituo kimya jinsi ilivyo hadi sasa katika alef ya Kiebrania. Hivyo walifanya picha kuwa herufi. Herufi ilinama jinsi kichwa cha ng'ombe kinavyoonekana kikitazamiwa kutoka kando.
Wagiriki walipokea alfabeti kutoka Wafinisia na pia jina la herufi hii. Hawakuwa na matumizi kwa ile sauti kimya ya Wafinisia lakini walihitaji herufi za vokali ambazo hazikuandikwa katika Kifinisia jinsi ilivyo hadi sasa katika Kiebrania na pia mara nyingi katika Kiarabu.
Kwa hiyo walitumia alama kwa sauti ya A wakabadilisha kidogo jina kuwa "alfa" badala ya "alef". Lakini katika lugha yao hawakuelewa tena maana asilia iliyokuwa "ng'ombe". Kwao ilikuwa alama ya sauti tu.
Mwanzoni waliandika herufi kwa umbo la kulala kama Wafinisia lakini katika karne za baadaye herufi iligeuzwa na kuandikwa mwishowe jinsi tunavyozoea leo.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article A, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.